NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wanufaika wa mradi wa kunusuru kaya maskini (TASAF) kwa kuuongezea muda mradi huo hadi mwaka 2025.

Ndejembi ameyasema hayo wakati akizungumza na wanufaika wa mradi huo Kata ya Rusimbi iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji mkoani Kigoma.

Amesema Rais Samia kwa mapenzi aliyonayo kwa watanzania ameamua kuuongezea muda mradi huo hadi mwaka 2025 ambapo awali mradi huo ulikua uishe mwaka 2023.

" Nimpongeze na nimshukuru Rais Samia kwa upendo aliouonesha wa kutuongezea muda wa mradi huu na sasa utaenda hadi mwaka 2025 badala ya mwaka 2023 ambapo ungemalizika. Hili ni jambo kubwa ambalo Hakika Rais wetu amelifanya kwa wanufaika wa TASAF.

Hivyo sasa ni wajibu wetu sisi wanufaika wa TASAF kuhakikisha tunatumia vema muda wa mradi huu kuboresha maisha yetu kwa kufanya mambo ya kimaendeleo kupitia fedha ambazo Serikali inawapatia ili kuondokana na umaskini.

Niwaombe sana Ndugu zangu tusimuangushe Rais wetu kwa yeye kutuongezea muda wa mradi huu, inabidi tumtie nguvu yeye kwa kutumia vema fedha hizi tunazopata ili tuweze kunyanyua maisha yetu na kuondokana na umaskini," Amesema Naibu Waziri Ndejembi.

Ametoa wito kwa waratibu wa TASAF kwenye kila Halmashauri kuendelea kutoa elimu kwa wanufaika wa mradi huo ili waweze kutumia kiasi cha fedha wanachopata kufanya miradi ya maendeleo ikiwemo kilimo, ufugaji na biashara ili siku mradi huo utakapokwisha kaya hizo ziwe zimeondokana na umaskini.

" Waratibu ni wajibu wenu kutoa elimu kwa watu wetu ambao ni wanufaika wa TASAF, kwa kufanya hivyo mtawasaidia kujiinua kiuchumi kwa fedha hizi wanazopata, niwasihi tena tumieni fursa hii ya Rais Samia kuongeza muda wa mradi kunyanyua maisha yenu, hilo ndio lengo la Serikali kuona wananchi walio katika kaya maskini wanajikwamua kiuchumi kupitia mradi huu," Amesemaa Naibu Waziri Ndejembi





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...