Mwanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha Ardhi jijini Dar es Salaam, Nyanzobe Makwaiya akizungumza leo Novemba, 14 2022 akizungumza alipozindua warsha ya siku tatu ya uongozi wa Kifeminia viongozi wanawake ikiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa uchambuzi wa Kifeminia na kuongeza uwajibikaji kwenye maeneo yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), akizungumza wakati wa warsha ya siku tatu ya uongozi wa Kifeminia viongozi wanawake ikiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa uchambuzi wa Kifeminia na kuongeza uwajibikaji kwenye maeneo yao.
Mtoa mada, Scholastica Makwaia akizungumza wakati wa warsha ya siku tatu ya uongozi wa Kifeminia viongozi wanawake ikiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa uchambuzi wa Kifeminia na kuongeza uwajibikaji kwenye maeneo yao.



Washiriki wa warsha ya siku tatu ya uongozi wa Kifeminia viongozi wanawake wakisikiliza mtoa mada jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2022.
Picha ya Pamoja.

MWANAMKE ni Mama Mwanamke ni Kiongozi muungoza njia ndivyo " ndivyo ambavyo unaweza kueleza kwa vielelezo mbalimbali pamoja na mfano wa wazi wa Rais Samia Suluhu Hassan amiri jeshi Mkuu wa Tanzania.

Rais Samia amewapa ujasiri wanawake wengi kuamini kuwa Mwanamke ni kiongozi bora kutokana na kurejesha matumaini nchini.

Mwanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha Ardhi jijini Dar es Salaam, Nyanzobe Makwaiya kwenye shahada ya kwanza ya Usimamizi wa Mazingira pia ni Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho anasema kuwa anaamini anaweza na kuwasihi wanawake wengine kusimama kwa kuwa tayati Rais Samia ameshatoa njia.

Hayo ameyasema leo Novemba, 14 2022 alipozindua warsha ya siku tatu ya uongozi wa Kifeminia viongozi wanawake ikiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa uchambuzi wa Kifeminia na kuongeza uwajibikaji kwenye maeneo yao.

"Nimekuja hapa kama Mgeni rasmi kwa ajili ya kufungua mafunzo ya uongozi kwa Wanawake ".

Anaeleza kuwa historia yake ya uongozi imeenza tangu alipoanza elimu yake ya awali mpaka sasa yupo Chuo kikuu akihudumu nafasi ya Uwaziri Mkuu.

Amesema kuwa amepata wito kutoka ndani ya nafsi yake lakini pia kutoka kwa watu wanaomzunguka.

"Kinachonisukuma kuwa kiongozi ni kuona kwama kunavitu vinafanyika katika namna ambayo pengine sio sahihi au sahihi lakini naweza kuboresha zaidi utendaji wangu ambapo watu waliokaribu yangu wanaona nafaa kuwania nafasi hiyo kwa hiyo nimepata msukumu kutoka ndani na kutoka kwa watu wanaonizunguka kuona kwamba ninafaa na kuona uwezo wangu katika kazi ninazozifanya." Amesema.

Ameleza mafanikio yake ni pamoja na kushiriki warsha mbalimbali na kitengeneza mtandao mkubwa wa kufahamiana na watu.

"Pia nimepata mafanikio ya kusaidia watu wengine kwa kuwa ukiwa kiongozi unatarajiwa kuwasaidia watu."

Ameeleza changamoto ni pamoja mifumo ya uongozi bado haijawa rafiki kwa mwanamke kwa kuwa anaongoza wanaume wenye fikra za kimfumo dume.

"Nafasi za uongozi nyingi zinachukuliwa na wanaume kuliko wanawake"

Changamoto nyingine ameeleza kuwa ni muda na fedha za kufanya kampeni.

Pamoja na changamoto zote hizo anasema kuwa wanawake wanaweza " wanawake ni jeshi kubwa wanaweka tunaweza hajalishi kuwa wewe ni kiongozi kwa sasa au sio kiongozi wanaweke tushaonesha nia na njia haijalishi umri wako unaweza unaweza kuamua leo kuanza na unaweza kufika unapotaka".

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Lihundi amesema kuwa Wanawake wapewa wito wa kuingia kwenye siasa ili kuingia kwenye nafasi mbalimbali za uamuzi nchini.

Amesema kuwa idadi ya wanawake kwenye ngazi za uamuzi hairidhishi hivyo amewataka wanawake wajitokeze kwenye nafasi za uongozi ili kuleta maendeleo kwenye jamii.

Amesema kuwa Mwanamke ndiye mwenye nafasi kubwa ya kuleta maendeleo kwenye jamii kwa kuwa wapo karibu zaidi kwenye jamii.

"Wanawake ni zaidi ya asilimia 50 ya wananchi Tanzania ndio maana tunasisitiza vijana wa kike na wanawake kwa ujumla wao washiriki kupata fursa au rasilimali hii ya uongozi.

Tumeambiwa na tafiti mbalimbali kuwa uongozi unaohusisha wanawake na wanaume unakuwa na tija kwa sababu macho ya wanawake yanaona vitu vingi zaidi kuliko macho ya wanaume unapozungumzia ukatili wa kijinsia kiongozi mwanamke atauona zaidi kuliko kiongozi Mwanamme unapozungumzia rushwa ya ngono kiongozi Mwanamke ataiona zaidi kuliko kuliko kiongozi mwanamme kwa sababu kiongozi mwanamke ndiye inayemuathiri Zaidi." Amesema Lilian.

Lakini kuna matatizo ya watoto na hata watu wazima kutokana na ile fursa mungu aliyotupa ya kuzalisha nguvu kazi na tunalea kwa hiyo unapomlea mtoto wa kike unapomlea mtoto wa kiume unawafahamu zaidi kwa hiyo unalea mtoto wa kike unalea mtoto wa kiume na unaishi na mwanamme ambaye ni mume wako ndugu zako kwa hiyo sisi wanawake tumepata bahati ya kuwajua wote ni rahisi kuzijua changamoto zao kiundani zaidi.

Amesema kuwa kuna changamoto ya wanawake kuwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi "kuna mila na Desturi zinazomfanya mwanamke asiwe kiongozi hata mfumo wa elimu ulivyotengenezwa hata kwenye vyuo vyetu hapa nchi kwenye nafasi za uongozi katika serikali za wanafunzi wapo wangapi, ukiingalia kwenye shule zetu za msingi na sekondari viongozi wa kike wapo wachache."

Amesema kuwa nafasi ya mwanamke kwenye uongozi kidunia hairidhishi kwa kuwa wapo viongozi wa juu wachache kwenye nchi zote duniani.

"Hata kwenye nafasi ya Urais unaona ni marais 21 tu kwenye nchi zote duniani ambapo ni wanawake akiwemo na Rais Samia kwa hiyo bado ni wachache mno"

Ameitaja nafasi ya kulisimamia bunge kwa wanawake kidunia amesema kuwa wanawake maspika wa Bunge duniani kote ni asilimia 20.9 huku manaibu Spika wakiwa 28.3 huku kwa wabunge wote duniani wanawake ni asimilia 25.5.

Amesema kuwa Tanzania imebahatika kuwa na wabunge wanawake asilimia 36.7 kutokana na kuridhia mikataba ya kimataifa pamoja na jitihada za wanaharakati.

Amesema kuwa Tanzania imepata bahati ya kipekee kwa kuwa na Viongozi wa Mihimili miwili ule wa Serikali yaani Rais ni Mwanamke (Rais Samia Suluhu Hassan) na ule wa Bunge (Spika ni Dk. Tulia Ackson).

Amesema kuwa asilimia ya wanawake kwenye ngazi ya maamuzi muhimu serikali za mitaa ni asilimia 2 tu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...