Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
Simba SC imemkana Kocha wa Makipa, Muharami Said Mohammed ambaye amehusishwa kuhusika kwenye uuzaji wa mihadarati.
Kwa mujibu wa taarifa ya Klabu hiyo iliyotolewa mapema leo, imeeleza kuwa Kocha huyo hakuwa Mwajiriwa kikosini hapo, huku ikieleza kuwa ilimuomba Muharami kuwanoa Makipa wa timu hiyo kwa muda wa mwezi mmoja wakati wakiendelea kutafuta Kocha mpya.
Aidha, Simba SC imesema kuwa haihusiki na tuhuma zinazomkabili Kocha huyo. Simba SC imewaomba Mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu kwani hakuna athari yoyote kwa Klabu kutokana na kadhia iliyomkumba Kocha huyo.
Mapema leo, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, kupitia kwa Kamishna Jenerali Gerald Kusaya ilithibitisha kuwa Kocha huyo amekamatwa na Kg 34 za Dawa za Kulevya aina ya Heroin.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...