Na Karama,Kenyunko, Michuzi TV

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imewashauri wazazi na walezi kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu vyakula wanavyokula Watoto kwani hivi sasa kumeshamiri uwepo wa vyakula ambavyo vimewekwa dawa za kulevya.

Kamishina Jenerali wa Mamlaka hiyo Gerald Kusaya amewaambia waandishi wa habari leo Novemba 15,2022 kwamba kuna wimbi kubwa la uwepo wa vyakula ambavyo vingi, ni vile vinavyopendwa na watoto kutengenezwa na dawa za kulevya,hivyo amewaomba Watanzania hasa wazazi kuwa makini na watoto wao.

Ameeleza kuwa kutokana na kushamiri huko kwa vyakula vilivyotengenezwa na dawa za kulevya ,wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa Abdulnasir Kombo(30) Mkazi wa Kaloleni jijini Arusha kwa kukutwa na biskuti 50 ambazo zimetengenezwa na dawa za kulevya aina ya bangi Pia wanamshikilia Hassan Ismail (25) anayetuhumiwa kutengeneza biskuti hizo.

"Matukio ya uwepo wa bidhaa za vyakula vinavyotengenezwa kwa kutumia bangi yameendelea kushamiri hasa kwa wafanyabiashara wenye nia ovu kwa kutumia vyakula vinavyopendwa na watoto kama pipi, keki Ice cream biscuits kuweka dawa aina ya bangi ndani yake,"amesema.

Ameongeza kuwepo kwa vyakula hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwaingiza watoto kwenye matumizi ya dawa za kulevya bila kujua na hatimaye kuwa waraibu. "Ninawataka wananchi kushiriki kwa dhati katika kukabiliana na tatizo la matumizi na biashara ya dawa za kulevya kwa kuwafichua wale wote wanaojihusisha ni biashara hiyo."


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...