WANANCHI waliotembelea maonyesho ya huduma za kifedha yanayoendelea jijini Mwanza yameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kwa kuleta mapinduzi katika huduma za kifedha na kuwezesha huduma hizo kupatikana kwa urahisi bila usumbufu.
Wakizungumza
katika nyakati tofauti walipotembelea banda la Maonyesho la TCRA
wananchi hao wamesema zamani kabla ya huduma za mawasiliano kuanzishwa
upatikanaji wa huduma za kifedha ulikuwa na changamoto ikiwemo kupoteza
muda, nauli kwenda kuzifuata na kutopatikana kwa taarifa za kifedha kwa
haraka tofauti na sasa ambapo kila kitu kiko kiganjani.
Bw.
Frederick Masanja amesema wakulima sasa wanapata huduma za kibenki
wakiwa huko huko mashambani tofauti na mwanzo kwamba walilazimika kwenda
mijini kufuata huduma.
Mwl.
Costa Mabula amasema zamani suala la mishahara kwao ilikuwa changamoto
tofauti na sasa ambapo upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya kisasa
imerahisisha na kupongeza TCRA kwa kuwezesha.
Katika
uwezeshaji sekta ya fedha TCRA inatoa leseni kwa makampuni yanayowekeza
katika huduma za miundombinu ya mtandao ambapo hadi sasa yapo 20,
makampuni ya huduma tumizi ambayo yapo 87na leseni za namba maalum za
huduma ambapo huduma za kifedha zimepewa namba zinazoanzia *150*
Wiki
ya huduma za kifedha zinaadhinishwa jijini Mwanza katika viwanja vya
rock city ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni elimu ya fedha kwa maendeleo
ya watu.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Mabel Masasi akitoa vitabu vya machapisho mbalimbali ya huduma zinatolewa na mamlaka hiyo kwenye maonesho ya wiki ya Fedha yanayofanyika kwenye Viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.
Wananchi wakisoma machapisho mbalimbali ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA kwenya maonesho ya Wiki ya Fedha yanayofanyika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...