Na Mwandishi Wetu
BILA Mshambuliaji wao mahiri, Romelu Lukaku, timu ya taifa ya Ubelgiji imefanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya timu ya taifa ya Canada kwenye dimba la Ahmed Bin Ali nchini Qatar.

Katika mchezo huo wa Kundi F, bao hilo la Ubelgiji limefungwa na Mshambuliaji wa timu hiyo, Michy Batshuayi kwenye dakika 44 ya mchezo, licha ya timu ya taifa ya Canada kuwasumbua Wabelgiji katika mchezo huo.

Hata hivyo, Canada walipata mkwaju wa Penalti kwenye dakika ya 10 ambapo walikosa mkwaju huo uliopigwa na Alphonso Davies, shujaa aliyepangua mkwaju huo ni Golikipa Thibaut Courtois.

Licha ya kumkosa Mshambuliaji Lukaku, Ubelgiji walikuwa na Nyota wake wengine, Kiungo Kevin De Bruyne, Batshuayi huku langoni wakilindwa na Golikipa mkongwe, Thibaut Courtois.

Awali, iliripotiwa kuwa Romelu Lukaku atakosekana kwenye michezo miwili ya Michuano hiyo, mchezo mmoja dhidi ya Canada na mchezo wa pili dhidi ya Morocco, kutokana na kuwa majeruhi wakati anaingia kwenye kambi ya timu hiyo nchini Qatar.

Ubelgiji wapo Kundi F na timu za Canada, Croatia na Morocco.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...