Na Mwandishi Wetu

Timu ya taifa ya Ujerumani imepoteza mchezo wake wa Michuano ya Kombe la Dunia baada ya kufungwa bao 2-1 na timu ya taifa ya Japan katika mchezo wa Kundi E uliopigwa katika dimba la Kimataifa la Khalifa mjini Doha nchini Qatar.

Katika mchezo huo, Ujerumani walipata bao la kuongoza kupitia kwa Kiungo, İlkay Gündoğan kwa mkwaju wa Penalti dakika ya 33. Kipindi cha pili, Japan walichachamaa na kusawazisha bao hilo kupitia kwa Winga Ritsu Doan dakika ya 75 huku bao la pili likifungwa na Mshambuliaji Takuma Asano dakika ya 83.

Kabla ya mchezo huo, Wachezaji 11 wa timu ya taifa ya Ujerumani waliziba midomo yao kwa mikono yao ya kulia, wakimaanisha kunyamaza bila kusema chochote kwa waandaji wa mashindano hayo ya dunia sanjari na Rais wa Shirikisho la Soka duniani (FIFA), Gianni Infantino aliyekuwa anashuhudia mchezo huo katika dimba hilo la Khalifa International, kutokana kuhamasisha Kampeni ya ‘Mapenzi ya Jinsia moja’ kupitia Michuano hiyo.

Shirikisho la Soka nchini Ujerumani kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, wamesema wanataka kutumia alama maalum (Armband) inayoashiria kuhamasisha ‘Mapenzi ya Jinsia moja’ ili kuunga mkono Kampeni hiyo na kuheshimiwa, kuungana pamoja na mataifa mengine yanayoshiriki Michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Hata hivyo, hivi karibuni Qatar walizuia Ndege ya Ujerumani iliyobeba Wachezaji wa timu hiyo kuingia nchini humo kutokana na kuwa na ‘Logo’ yenye ujumbe unaohamasisha ‘Mapenzi ya Jinsia moja’, Ndege hiyo ililazimika kutua uwanja wa Ndege wa Oman ambapo ilibadilishwa na kuja Qatar bila ujumbe huo.

Baadhi ya mataifa ya bara la Ulaya yanaunga mkono Kampeni hiyo ya ‘Mapenzi ya Jinsi moja’. Nchi za Falme za Kiarabu kukakaa na kupinga utamaduni huo wa mataifa hayo ya Ulaya

Waziri wa Mambo ya Ndani na Jamii katika Shirikisho la Ujerumani, Nancy Faeser (Kulia) akiwa amevalia ‘armband’ Kushoto ni Kiongozi wa Shirikisho la Soka nchini Ujerumani, Bernd Neuendorf wakishuhudia mchezo baina ya timu yao ya taifa ya Ujerumani dhidi ya timu ya taifa ya Japan kwenye dimba la Khalifa International.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...