*Achaguliwa kwa kura 358, mpinzani wake aambulia kura 38 pekee.
*Wagombea wengine wawili waingia mitini.

WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake CCM Mkoa wa Pwani wamemchagua aliekuwa Mbunge wa Viti maalumu Pwani Mhe. Zaynab Matitu Vulu kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa huo.

Mhe. Vulu ameshinda nafasi hiyo kwa kupata jumla ya kura 320 Kati ya kura 358 zilizopigwa akifuatiwa na Joan Tandau aliepata kura 38 pekee huku wagombea wawili waliokuwa wakiwania nafasi hiyo wakiingia mitini na kupata kura sifuri.

Katika uchaguzi huo idadi ya kura zilizopigwa ni 358 na hakuna kura iliyoharibika.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Mhe. Zaynab Matitu Vulu amewashukuru wajumbe kwa Imani kubwa na dhamara waliyompatia ambapo amewaahidi kuendelea kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...