Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.
Selemani Jafo amepokea Taarifa fupi ya usafishaji wa Mto Msimbazi kutokana na
maelekezo aliyotoa hivi karibuni kwa Kikosi cha kuratibu usafishaji Mito na
Mabonde Mkoa wa Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imewasilishwa kwa Waziri Jafo ofisini kwake jijini Dodoma na
Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuratibu usafishaji wa Mito na Mabonde Mkoa wa
Dar es Salaam Dkt. Elizabeth Mshote.
Hivi karibuni alifanya ziara ya kikazi ya kukagua mto huo katika Kata ya Mogo
Mtaa wa Kipawa baada ya kupokea malalamiko kuhusiana na athari za
kimazingira zinazotokana na usafishaji wa mto huo.
Hata hivyo, wakati wa ziara hiyo baada ya kusikiliza maoni ya wananchi alipata
maoni yanayokinzana ambapo wengine walidai shughuli za usafishaji mto huo
zimeleta athari kwa mazingira na wengine wakidai zimeleta manufaa makubwa
kwa jamii inayozunguka eneo hilo.
Itakumbukwa Februari 2021 Waziri Jafo alikutana na wadau wanaojishughulisha
na uchimbaji mchanga katika mkoa huo kujadili changamoto za kimazingira
zinazotokana na uchimbaji mchanga kiholela kiholela katika mito na mabonde ili
kuweka utaratibu mzuri.
Kikao hicho kiliwezesha kuandaliwa Mwongozo wa usafishaji mito utakaotumika
katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuondoa mchanga, taka ngumu na
tope ili kupunguza au kuondoa madhara ya mafuriko ambao ulitolewa kwa
mujibu wa kifungu cha 57 (2) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka
2004.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikabidhiwa Taarifa fupi ya Usafishaji wa Mto Msimbazi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuratibu usafishaji wa Mito na Mabonde Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Elizabeth Mshote alipowasilisha ofisini kwa Waziri jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.Selemani Jafo akipitia Taarifa fupi ya Usafishaji wa Mto Msimbazi mara baada yakuipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha kuratibu usafishaji wa Mito na Mabonde Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Elizabeth Mshote na Kikosi chake walipowasilisha ofisini kwa Waziri jijini Dodoma.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...