Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo wilaya ya Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mradi huo unafika katika Jiji la Dar es Salaam ili kupunguza makali ya upatikanaji wa maji kwenye Mkoa huo.
Wazii mkuu amesema jana alipokea maagizo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokuwa anazungumza kwenye Kongamano la Kitaifa la Nishati Safi ya Kupikia ambapo aligusa upatikanaji wa majilakini pia akaja kuzungumza upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa na kuagiza kutaka maelezo ya kina kuhusu changamoto hiyo.
"Sasa hivi tuna tatizo la upatikanaji wa maji kwenye Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ambapo Mikoa hiyo inategemea chanzo Kikuu cha mto Ruvu lakini pia kwa Kigamboni tunategemea visima hivi hivyo kutokana na changamoto hizi naagiza DAWASA kuhakikisha wanafanya kazi kwa masala 24 ili kuhakikisha maji yanaanza kupatikana kwa kutumia chanzo cha Kigamboni" alisema Majaliwa
Amesema Jiji la Dar es Salaam lina mahitaji ya maji Lita Milioni 540 lakini kama tunakuwa na mvua za kutosha basi kutakuwa na uwezekano wa kupata maji Lita Milioni 520 tukiwa na upungufu wa Lita Milioni 20 lakini kwa sasa Jiji la Dar es Salaam linapata Lita Milioni 300 ikiwa na upungufu wa Lita Milioni 220.
Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha maeneo yote yanapata huduma za maji na kazi ya uchimbaji visima pamoja na kutafuta vyanzo vingine vya maji inaendelea ili kufikia matamanio ya Mheshimiwa Rais Samia ya kufikisha huduma ya maji karibu na makazi ya wananchi.
Akizungumza baada ya kukagua na kuwasha pampu ya maji katika mradi wa Visima vya Maji kwenye mradi wa Kisarawe II uliopo Kigamboni, Waziri Mkuu amesema visima hivyo ambavyo vinauwezo wa kuzalisha maji lita milioni 70 kwa siku vitasaidia katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar Es Salaam.
“Katika kipindi hiki ambacho kiwango cha maji katika Mto Ruvu kimepungua uzalishaji wa maji nao umepungua na kufikia lita milioni 300 kwa siku, hivyo kusababisha upungufu wa lita milioni 244. Kwa sasa tukiingiza lita milioni 70 kutoka katika mradi huu wa visima vya Kigamboni tutakuwa na upungufu wa lita milioni 174, hivyo tutaupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji katika baadi ya maeneo.”
Waziri Mkuu amesema katika mwaka wa fedha 2021/2022 Mheshimiwa Rais Samia alitoa shilingi bilioni 25 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa uchimbaji visima 10 katika eneo la Kigamboni, ambapo kati yake visima saba ndio vimewezesha upatikanaji wa lita milioni 70. Amewaagiza watendaji DAWASA waendelee na uchimbaji wa visima vingine.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akishika maji mara baada ya kuzindua maji kwa ajili ya wakazi wa Kigamboni na Dar es Salaam alipotembelea mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha maji ya Kigamboni yanafika Dar es Salaam ili kupunguza makali ya mgao wa maji.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akifungua koki ya maji kuashiria uzimduzi wa maji wa Kisarawe II kwa ajili ya wakazi wa Dar es Salaamwakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha maji ya Kigamboni yanafika Dar es Salaam ili kupunguza makali ya mgao wa maji.
Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza kuhusu namna wanavyoendelea na jitihada za kupunguza ukali wa mgao kwa kuhakikisha wanapeleka maji Dar es Salaam kwa kutumia mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ya kukagua maendeleo ya mradi huo Pamoja na kuzindua maji yatakayotumika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla akizungumza kuhusu kupokea maagizo aliyopewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa alipokagua maendeleo ya mradi wa maji wa kukagua ujenzi wa Tanki, uchimbaji wa visima kwenye mradi wa maji wa Kisarawe II katika wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa moja ya visima vinavyozalisha maji kwenye mradi wa Kisarawe II wakati wa ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wakazi wa Dar es Salaam wanapata maji kutoka kwenye mradi huo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mradi wa Kisarawe II walipotembelea Tanki la maji la Kisarawe II lenye ujazo wa Lita Milioni 15 linalojengwa na DAWASA lililopo Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II hii ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza jambo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuhusu mradi wa Kisarawe II walipotembelea Tanki la maji la Kisarawe II lenye ujazo wa Lita Milioni 15 linalojengwa na DAWASA lililopo Wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi pamoja na waandishi wa habari wakati wa kutembelea mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kujionea maendeleo ya mradi huo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu ya kuhakikisha maji ya Kigamboni yanafika Dar es Salaam ili kupunguza makali ya mgao wa maji.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso pamoja, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama wakiendelea na ziara ya kukagua mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wakazi wa Dar es Salaam wanapata maji kutoka kwenye mradi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...