Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Ni rasmi sasa timu ya taifa ya Uholanzi itacheza hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Argentina baada ya timu hiyo kupata ushindi mabao 2-1 katika mchezo wa hatua ya 16 Bora, dhidi ya Australia kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Ahmed Bin Ali.
Nahodha wa Argentina, Lionel Messi amefanikisha hilo la kuiongoza timu hiyo kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia, baada ya dakika ya 36’ Messi kuifungia timu hiyo bao la kwanza baada ya kuubura mpira katikati ya safu ya ulinzi ya timu ya Australia.
Argentina hawakutosheka na bao hilo waliongeza bao la pili kupitia kwa Julián Álvarez dakika ya 57’ baada ya makosa ya Golikipa wa Australia, Mathew Ryanwakati akitaka kuondoa mpira huo kwenye eneo lao. Hata hivyo, Australia walipata bao moja baada ya Enzo Fernández kujifunga mwenyewe.
Nahodha Lionel Messi amefunga mabao 789 kwenye michezo 1000 ambayo amecheza katika ngazi za Klabu na timu ya taifa. Safari ya Nahodha Lionel Messi inaendelea katika Michuano ya Kombe la Dunia ambapo Desemba 9, 2022 watacheza dhidi ya Uholanzi katika hatua hiyo ya Robo Fainali.
Uholanzi walifuzu hatua ya Robo Fainali baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya taifa ya Marekani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...