Na Mwandishi Wetu
Wadau wa ufugaji wa kuku nchini wameonesha imani kwa serikali ya awamu
ya sita inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan katika kusaidia
kulinda soko la ndani la uzalishaji wa vifaranga.
Wakizungumza katika mdahalo ulioshirikisha wazalishaji wa vifaranga wa
ndani ya nchi mawakala wa uuzaji wa vifaranga pamoja na wafugaji, kwa
pamoja wadau hao walieleza kuwa uingizwaji wa vifaranga hivyo umekuwa
na athari kiuchumi.
Akizungumzia uingizwaji huo wa vifaranga Mkurugenzi wa Kampuni ya
Organia inayozalisha vifaranga hapa nchini, Albert Momdjian
alibainisha kuwa kumekuwa na wimbi la uingizwaji wa vifaranga kwa njia
zisizokuwa za halali kutoka nchi jirani hususan Kenya na Malawi
ambavyo huuzwa sokoni kwa bei rahisi.
Alisema,” vifaranga vinavyoingizwa nchini hasa vile vua njia
zisizokuwa halali vimekuwa na athari kubwa kwa wazalishaji wa
vifaranga wa ndani hasa kutokana na kuleta ushindani usiokuwa sahihi,
wao wanaweza uza hata kwa bei ya chini sababu hawaingia gharama za
kodi katika kuingiza.”
“Ni imani yangu kuwa chini ya serikali ya Rais Samia kila kitu
kinaenda kuwa sawa hasa wahusika watachukuliwa hatua kwa kuwa wapo
wanaoingiza kwa njia ya mabasi huku wengine wakiuza hadharani iwe eneo
la Tazara na kwengineko” aliongeza Momdjia.
Pia alisema kuwa kwa kampuni zinazopewa vibali vya kuagiza vifaranga
nje ya nchi na zenyewe zinatakiwa kudhibitiwa kwa kuwa zipo nchi kama
Marekani na nyingine za ulaya zilijikuta zikiingiza magonjwa kwenye
nchi zao kutokana na kuruhusu vifaranga kutoka nje ya nchi zao ambavyo
vilikuwa na magonjwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji wa Kuku Tnazania
(TABROFA) Costa Mrema alibaisha kuwa kutokana na kuwepo kwa idadi
kubwa ya watanzania kujiajili kwenye ufugaji wa kuku, ni vema suala la
kuingizwa kwa vifaranga vya nje likaangaiwa kwa umakini zaidi.
Alisema “sera ya nzuri ya Rais Samia imepelekea kuja kwa wawekezaji
wakubwa kutoka nje kufika kuwekeza kwenye uzalishaji wa vifaranga kama
hii kampuni ya Organia ambao wanalenga kuzalisha vifaranga na kuuza
nje ya Tanzania hivyo kuna kila sababu ya kuzuia vifaranga vya nje ili
kulinda soko la ndan”
Naye mfugaji wa kuku, Mwajuma Rajabu alibainisha kuwa vifaranga vya
nje vimekuwa vinaharibu ufugaji wa kuku nchini kwa kuwa kutokana na
kuingizwa kwa njia za panya wafugaji wa kuku ambao wananunua vifaranga
hivyo wamekuwa wavifuga na kisha kuuza kuku kwa bei ya chini kwa kuwa
wananunua vifaranga vya magendio vinavyouzwa kwa bei ya kawaida.
“Mimi ninaamini kuwa Rais huyu ni Dk Samia ni msikivu na mtenda haaki
hivyo anasikia na atasaidia kutusikiliza kwa kuhakikisha serikali yake
inakabiliana na uingizwaji wa vifaranga kihoela” anasema Mwajuma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...