Na Jane Edward,Arusha

Kampuni ya Equiplus inayojihusisha na usambazaji wa vifaa vya maji imewataka wananchi wake kutumia bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo kwani zina ubora wa hali ya juu.

Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, James Genga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma hizo wanazotoa .

James amesema kuwa,vijana wa kitanzania asilimia 100 wamejikita kusaidia sekta ya maji kwa kusambaza pump za maji na kuzifunga katika mikoa mbalimbali nchini.

Amesema kuwa,kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 2018 ambapo wamekuwa na mafanikio makubwa kwani wamekuwa wakifanya kazi na wizara ya maji na mamlaka za maji na hiyo ni kutokana na huduma nzuri wanayotoa kwa wateja .

Naye Meneja mkuu wa kampuni ya SBS Tanks ,Robert Tunje amesema kuwa,kampuni hiyo imekuwa ikijenga matanki ya maji kwa kutumia Zink na aluminium ambayo inadumu kwa muda wa miaka 65.

Amesema kuwa, matanki hayo yana ubora wa hali ya juu tofauti na nyingine kwani hayapati kutu kama yalivyo matanki mengine na wamekuwa wakiyajengea viwandani ,majumbani,na kwenye machimbo ya madini ambapo yameleta manufaa makubwa sana kwao.

"Matanki hayo tayari tumeshajenga katika mkoa ya Tanga,Kilimanjaro, Shinyanga ambapo asilimia kubwa ambao tumewajengea ni mamlaka za maji na hiyo ni kutokana na ubora wa hali ya juu tulionao."amesema.

Uongozi wa SBS Tanks wakiwa kwenye banda lao katika mkutano uliowajumuisha wadau wa sekta ya maji jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya EQUIPLUS James Genga akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Mshiriki wa Mkutano akifafanua jambo.
Robert Tunje meneja Mkuu akifafanua jambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...