Na Jane Edward,Arusha

Wawekezaji wanaoshindana katika sekta ya viwanda,ndege na makampuni ya utalii wametakiwa kutumia teknolojia rafiki ili kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa inayochangia mabadiliko hasi ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa jijini Arusha na Naibu Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe wakati wa ufunguzi wa kongamano la madhimisho ya Ushindani Duniani katika kilele cha siku ya ushindani Duniani.

Alisema endapo endapo kampuni hizo zitazingatia matumizi sahihi ya matumizi ya hewa ukaa itasaidia kupunguza hewa ukaa inayochangia mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema lengo la wafanyabiashara wote ni kupata faida hivyo lazima kuhakikisha ushindani wa haki unazingatiwa ikiwemo kuhakikisha mamlaka ya ushindani zinazuia ukiritimba katika biashara ikiwemo nguvu ya soko kuwameza washindani katika biashara.

Pia kudhibiti muingiliano wa biashara katika unaolenga kuwaweza washindani katika baadhi ya biashara na kuongeza kuwa ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi unahatarisha usalama na uhatarishi wa theluji katika mlima Kilimanjaro.

"Wawekezaji katika sekta ya Viwanda,ndege na makampuni ya utalii kutumia teknolojia rafiki katika kudhibiti mazingira ikiwemo wanyama katika sekta ya utalii katika upunguzaji wa ikolojia ya wanyama ikiwemo ukataji ovyo wa miti ikiwemo mkaa "alisema Kigahe.

Alitoa rai kwa wadau mbalimbali kupanda miti ili kudhibiti uongezeko la hewa ukaa hivyo ni lazima miti ipandwe katika kulinda ikolojia ya wanyama sanjari na uoto asili

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC),Dk,Aggrey Mlimuka alisema kuwa, kongamano hilo ni muhimu katika kuhakikisha kunakuwa na uendelevu na ushindani katika kuhakikisha utalii unakua kwa kasi sanjari na ulinzi wa mazingira

"kauli mbiu ya mwaka huu ni ushindani na maendeleo endelevu kwani kuwepo kwa Utalii huo endelevu kuna hitaji juhudi za pamoja katika kulinda mazingira ikiwemo ufanyaji biashara na kuleta ushindani."alisema

Naye Jaji Salma Maghimbi kutoka Baraza la Ushindani alitoa rai kwa mawakili kuhakikisha wanazingatia kanuni na sheria katika uendeshaji wa kesi za ushindani katika kuhakikisha kesi zinasikilizwa na kutolewa maamuzi.

Awali Kaimu Mkuu wa wilaya ya Arusha,Injinia Richard Ruyango alitoa rai kwa wadau mbalimbali katika sekta ya mazingira kuhakikisha mazingira yanalindwa ili kuzuia chagamoto za mabadiliko ya tabia nchi na ikolojia.

Naibu waziri wa uwekezaji Viwanda na biashara Exaud Kigae akifungua mkutano wa Tume ya ushindani jijini Arusha.

Mkurugenzi Mkuu FCC William Erio akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Tume ya ushindani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...