Na Jane Edward, Arusha


Maadhimisho ya siku ya ushindani
Duniani wa kibiashara katika kukuza uchumi wa kimaendeleo unatarajiwa kufanyika jijini Arusha huku zaidi ya washiriki 120 kuhudhuria Mkutano huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni Sera ya ushindani na mabadiliko ya Tabia nchi.

"FCC kama taasisi ya serikali tumepewa jukumu la kuratibu Shughuli zote za ushindani na tumetohoa kauli mbiu hiyo na Ushindani na utalii endelevu,na wadau wa sekta ya utalii kutoshiriki kuharibu mazingira "Alisema Erio

Amesema Desemba 5 ndiyo siku iliyokubaliwa kimataifa kuwa ni siku ya ushindani Duniani lengo likiwa ni kuhakikisha uchumi wa dunia unakuwa pamoja na biashara .

Ameongeza kuwa FCC inawajibu wa kuhakikisha kuwa na ushindani halali ambapo katika kuunga mkono kauli mbiu sekta ya utalii ndio wadau wakubwa wa kuhakikisha uharibifu wa mazingira unadhibitiwa.

"Tumeitisha kikao cha wadau wa mazingira na wadau wa utalii ili kuangalia kwa pamoja ni namna gani shughuli zetu haziathiri hewa ukaa ikiwemo mlima Kilimanjaro ili kutopoteza watalii katika maeneo hayo"Alisema

Amesema FCC imekuwa ikifanya makongamano mbalimbali katika vyuo na Mkutano huu unalenga kusaidia kutoongezeka Hewa ukaa pamoja na theluji iliyopo kwenye Mlima Kilimanjaro.

Amesema mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kuwa na athari mbalimbali katika ikolojia na kuharibu maeneo wanayoweza kuishi wanyama na hivyo kukutana wadau kutarahisisha kuona namna gani wanaweza kupunguza changamoto hiyo.

Aidha Katika mkutano huo wanatarajia kuwepo kwa mawaziri wa sekta mbalimbali huku mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa waziri wa uwekezaji Dkt Ashatu Kijaji.

Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...