Mshindi wa Kampeni ya MastaBata KoteKote, Bernard Matiku (kulia)
akipokea funguo ya pikipiki kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa –
Baraka Ladislaus wakati wa hafla ya kukabidhiwa. Kushoto ni Mkuu wa
Idara ya Biashara ya kadi wa NMB – Philbert Casmir.
Mshindi
wa Kampeni ya MastaBata KoteKote, Bernard Matiku(wa pili kushoto)
akibonyeza kitufe ili kuwapata washindi wengine wa kampeni hiyo.
Wakishuhudia; Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya Kadi wa NMB-
Philbert Casmir, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Baraka Ladislaus(wa tatu
kushoto) na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha – Erick
Mremi(kulia).
*****************
nne wa promosheni ya NMB
MastaBata kwa ajili ya kuchagiza matumizi ya kadi za malipo za
kidijitali umezidi kunoga baada ya kundi la kwanza la washindi 51 wa
kila mwezi kupatikana katika droo iliyofanyika kwenye tawi la NMB
Kenyatta mkoani Mwanza wiki hii, ambapo 49 walijishindia pesa taslimu
TZS 1,000,000 kila mmoja na wawili wakishinda pikipiki aina ya Boxer.
Lengo
la kampeni hii ya MastaBata KoteKote ni kuhamasisha matumizi ya kadi ya
NMB Mastercard na Lipa Mkononi (Mastercard QR) kwa wateja wetu
wanapofanya malipo kwenye manunuzi yao.
Mkazi wa Bunda jijini
Mara, Bernard Lucas Matiku alisema ‘Asante sana Benki yangu ya NMB kwa
kunizawadia pikipiki, nimeanza vizuri msimu huu wa sikukuu maana sasa
sina wasiwasi kuendesha mishe zangu’ baada ya kukabidhiwa pikipiki
aliyoshinda katika promotion ya NMB MastaBata KoteKote.
Zoezi
hilo lililosimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania
limepelekea idadi ya washindi wa kampeni ya NMB MastaBata KoteKote
kufikia 225 hadi sasa. zawadi walizoshinda wateja hao kwa siku hii zina
thamani ya zaidi ya TZS milioni 55 huku shindano zima likiwa na thamani
ya zaidi ya TZS milioni 300.
Zawadi za kila wiki zitakuwepo
ambapo jumla ya washindi 75 watanyakua pesa taslimu TZS 100,000 kila
mmoja na mmoja zawadi ya Pikipiki (boxer), kwa mwezi jumla ya washindi
98 watanyakua pesa taslimu TZS 1,000,000 kila mmoja huku kila mwezi
kukiwepo zawadi ya Pikipiki (Boxer) mbili. Zawadi ya droo ya mwisho ni
safari ya siku nne huko Dubai kwa washindi saba na wenza wao.
Endelea
kufanya malipo kwa kutumia NMB mastercard au Lipa Mkononi (mastercard
QR) ujiwekee nafasi ya kushindia zawadi kibao na #NMBMastaBataKoteKote
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...