Na Mwandishi Wetu, Pwani

CHUO cha Ufundi Stadi (VETA ) Mkoa wa Pwani, kimewaomba wahisani na wadau kuwasaidia vijana wenye mahitaji maalumu walioko mitaani kujiunga na chuo hicho, kupata ujuzi na kujiajiri kwa lengo la kuendana na kasi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza sera ya kulifikisha taifa katika uchumi wa viwanda.

Pia, wahitimu katika chuo hicho wamesisitizwa kutumia taalumu waliyoipata kufikia malengo yao badala ya kwenda katika jamii na kufanya kazi isiyoendana na taaluma waliyonayo.
Hayo yamejiri katika Mahafali ya 10 ya chuo hicho, kilichopo katika eneo la Kongowe, Mlandizi mkoani Pwani.

Akiwatunuku vyeti wahitimu 99 wa ngazi ya pili katika chuo hicho, Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Keda (T) Ceramics Co. LTD, Chen Ziao Wei, amesema, kwa sasa Tanzania ina kasi kubwa ya uwekezaji katika sekta ya viwanda hivyo vijana wenye taaluma wanayo nafasi kubwa ya kuajiriwa.

Mwekezaji huyo kutoka nchini China ambaye amewekeza kiwanda katika Halmashauri ya Mji Mdogo wa Chalinze mkoani humo, amesema kampuni yake iko tayari kuchukua vijana wengi wanao hitimu katika chuo hicho na kuwaajiri, pamoja na kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazo kikabili chuo hicho.

“Ninaamini kozi zinazotolewa hapa ni bora na nimeona vifaa vya kisasa vya kufundishia. Mna walimu wazuri hivyo taaluma mliyoipata itawasaidia kujiajiri na hata kuajiriwa katika kampuni yetu na kampuni zingine zinazoanzishwa hapa nchini. Sisi tuko tayari kuchukua wahitimu kutoka hapa hivyo muwe huru kutuona na tutawasaidia,”amesema.

Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Pwani, Wilhard Soko, aliwataka wazazi na walezi mkoani Pwani kukitumia chuo hicho vizuri kwa kuwapeleka vijana wao kujiunga na chuo hicho.

Pia amewataka wahitimu kutumia taaluma zao kwa manufaa yao na taifa badala ya kubadilisha shughuli za kufanya wawapo mtaani.

“Katumieni taaluma mliyopata hapa. Ukiacha kutumia taaluma uliyoipata na kufanya shughuli nyingine ukija kuulizwa umesoma wapi usiseme umesoma VETA Pwani. Tumieni ufundi mlioupata hapa kwa manufaa yenu,”alimesema Soko.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha VETA Pwani, Clara Kibodya, ameitaka a jamii kufadhili vijana walio katika mazingira magumu kusoma katika chuo hicho kupata mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali.

“ Serikali imefanya kwa sehemu kubwa lakini bado wapo vijana wengi mitaani wanahitaji kupata mafunzo hayo na kujiajiri au kuajiriwa. Ninaamini kwa njia hii tutakuwa tumeunga mkono kauli mbiu ya serikali inayoongozwa na Rais Samia kuendeleaza kujenga nchi ya uchumi wa viwanda,”amesema Clara.

Ameeleza wapo vijana mitaani wanaoshi katika mazingira magumu, hivyo wahisani wanahitajika kuwasaidia kujiunga na chuo hicho.
Akizungumzia kuhusu mahafali hayo ya Clara amesema jumla ya wahitimu ni 99, wavulana 62 na wasichana 37 ambao wamehitimu katika ngazi ya pili.

“Wamehitimu katika fani za uselamala, ufundi wa vifaa vya umeme, ushonaji na ubunifu wa mitindo, ufundi wa magari na usaidizi wa maabara,”alibainisha.

Alisema, wamesoma kwa umahili, nadharia na vitendo kisha kwenda kusoma kwa vindendo katika viwanda kwa muda wa miezi mitatu, hivyo wanaujuzi unawaowafanya kuajirika au kujiajiri.

“Mafunzo ya VETA ni ufundi mahili, unaolenga kuzingatia ujuzi wa soko la ajira,”alisema Clara. Aliomba pia wahisani kusaidia chuo hicho kutatua changamoto ikiwemo ya upungufu wa mabweni, vyumba vya madarasa, samani na ujenzi wa barabara bora inayoingia chuoni hapo kutoka Barabara ya Morogoro.
 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...