Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SERIKALI ya Tanzania imeahidi kuendeleza ushirikiano na jirani yake Kenya kupitia Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission JPC) ambayo ni daraja pekee katika kukuza mahusiano ya kikanda yanachochea ukuaji wa kiuchumi, kibiashara na kijamii.
Akizungumza kwa niaba ya Tanzania kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Kenya , Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Damas Ndumbaro amesema Tanzania inaungana na nchini zingine duniani kusherehekea historia ya Kenya na mabadiliko makubwa waliofanya tangu kupata uhuru.
Amesema kupitia Tume hiyo ambayo ni kichocheo cha kuvumbua maeneo mapya ya mapya ya mahusiano ya kibiashara na uwekezaji kwa manufaa ya nchini hizo mbili.
“Nachukua nafasi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan kuwapongeza ndugu zetu Wakenya kwa kutimiza miaka hii 58 tangu kupata uhuru na mafanikio makubwa walioyapata ya kijamii, kiuchumi na kisiasa,” amesema.
Ameongeza kuongezeka kwa ukuaji wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ni kielelezo cha kutosha kwamba kunahitajika juhudi zaidi katika kuongeza uwekezaji na kuweka mazingira mazuri na salama kwa wafanyabiashara wa nchini hizo mbili kuendelea kufanya biashara.
“Nachukua nafasi hii kuwahakikishia ndugu zetu Wakenya kwamba Tanzania itaendelea na ushirikiano wa karibu na majirani zake katika juhudi za kukuza uchumi na ustawi wa maisha ya watu wa nchini hizi mbili,” aliongeza
Kwa upande wake Balozi wa Kenya hapa nchini, Isaac Njenga amesema furaha ya Desemba 12 ni kwamba wanasherehekea hatua mbili muhimu za safari yao ya uhuru - ni siku ambayo Kenya ilipata Uhuru mnamo 1963 na pia ni siku ambayo Kenya ilibadilika na kuwa jamhuri kamili au Jamhuri mnamo 1964-mwaka mmoja baadaye.
“Tunajivunia mafanikio mengi ambayo tumeyapata kama Taifa, tumejenga nchi yenye utambulisho na tabia. Mnamo Agosti mwaka 2010, Kenya ilipitisha Katiba mpya,”
“Katiba ya Kenya ya 2010 ni miongoni mwa katiba bora zaidi duniani zinazohakikisha haki za kimsingi za kibinadamu na kuwapa raia mamlaka makubwa ya kuamua jinsi wanavyopaswa kutawaliwa,” amesema Balozi Njenga.
Ameongeza uchaguzi wa tatu chini ya Katiba mpya ulifanyika tarehe 9 Agosti mwaka huu ambapo Mheshimiwa Mhe. William Samoei Ruto alichaguliwa kuwa Rais wa 5 wa Jamhuri ya Kenya.
“Chaguzi hizi pia ziliashiria mabadiliko mengine ya amani- ambapo tulionyesha ukomavu wa demokrasia yetu, uimara wa taasisi zetu ambazo zilitimiza matarajio yetu na uthabiti wa watu wa Kenya. ”
Pamoja na mambo mengine amesisitiza ustawi wa nchini yao unategemea ushirikiano na majirani zao , udugu na ushirikiano na Jumuiya ya kimataifa.
Amesema katika nyanja hizo zote, Kenya itaendelea kuwa mshirika wa kutegemewa, rafiki mwaminifu na mshirika mwaminifu, aliyewahi kujitolea kushinda na kupata matokeo ya pande mbili na ya kimataifa, ambayo yanaafiki mafanikio ya pande zote kwa manufaa ya binadamu.
Ameongeza Kenya imeendelea kukua kiuchumi ambapo pato la Taifa (GDP) linatarajiwa kukua zaidi kwa asilimia 5.5 mwaka 2022 licha ya changamoto zinazotokana na Janga la Uviko-19 na kuongezeka kwa bei za bidhaa muhimu duniani.

Cheerrrsssss... kuimarisha na kudumisha umoja


Mgeni rasmi Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Damas Ndumbaro akisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo


Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mhe.Isaac Njenga akiwakaribisha wageni wake mbalimbali











Makamu Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Tanzania Bara,Kanali Mstaafu Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk.Damas Ndumbaro aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje Dkt. Stergomena Tax
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...