KADA Mbobevu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Chacha Wambura ameshinda ujumbe wa Halmashauri Kuu kwenye nafasi 20 Tanzania Bara.

Wambura ameyasema hayo kwa njia ya simu kuhusiana na ushindi huo uliopatikana katika uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika kwa siku mbili mjini Dodoma.

Wakati akiomba kura alisema amekuwa ndani ya Chama kwa muda mrefu na kushika nafasi mbalimbali ambazo ameweza kuzimudu kwa uaminifu na na maarifa yake ya kufanya chama kisonge mbele.

Mbali na kuwa Mwana CCM Wambura ni Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ua WAJA Group na kuamini kuwa anatosha kwenye nafasi hiyo.
Amewashukuru Wajumbe kwa kuwa na imani yake katika harakati za kuhakikisha chama hicho kinasonga mbele kwa kuendelea kushika dola.

WAJA ni mwekezaji kwenye viwanda vya chuma kupitia Waja Mabati, Uchimbaji wa Madini pamoja na sekta ya Elimu ambapo ana shule ya Waja Boys, Girls na Primary schools . Pia amewekeza kwenye sekta ya afya ambapo ana vituo vya afya, pamoja na Waja Hospitali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...