Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imefanya kikao cha Baraza la wafanyakazi leo ili kujadili mafanikio, mafanikio, changamoto na njia za kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza kwenye upangaji wa bajeti ya mwaka ya 2022/2023 ikiwa ni pamoja baraza hilo kupitisha dodoso bajeti mpya ya mwaka mpya wa fedha.
Akizungumza kwenye kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu Ununuzi na Ugavi Godfred Mbanyi amesema baraza ni chombo kinachoundwa na sheria ya Mahusiano kazini kwa ajili na kuweka mazingira mazuri mahali pakazi ambapo chombo hiki kinawiwa kwa mkataba baina na Menejimenti pamoja na chama cha wafanyakazi sehemu ya kazi.
Pia amasema baraza la leo limefanyika ili kutathmini utendaji kazi wa bajeti ya mwaka ya 2022/2023, kisheria na kiutaratibu bajeti yoyote kabla haijahidhinishwa lazima ipitishwe na Balaza la Wafanyakazi sehemu ya kazi.
Mbanyi amesema Bajeti ya mwaka 2022/2023 itakamilika Juni 30 mwaka 2023 hivyo ni wajibu wa menejimsenti kuja kueleza balaza nini mafanikio, changamoto na njia za kuweza kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa bajeti itakayokamilika Mwezi Juni 30 mwaka huu.
“Umuhimu wa Mabaraza ya kazi kwanza yanaleta ushirikishwaji wa wafanyakazi sehemu ya kazi hivyo wafanyakazi wanakuwa ni sehemu ya maamuzi katika taasisi, kwaiyo taasisi sio kwamba inakuwa inaongozwa na Menejimenti lakini inakuwa na chombo ambacho kinawakilisha wafanyakazi wote katika taasisi mbalimbali.” Alisema Mbanyi
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa kufungua kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB kilichokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi pamoja na kujadili mafanikio, mafanikio, changamoto na njia za kuweza kutatua changamoto hiyo kilichofanyika leo Kibaha mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa TUGHE PSPTB, Shilla Mwandu( wa kwanza kushoto) akizungumza kuhusu namna wafanyakazi wanabidi kujitadhmini pale wanapokuwa wanafanya kazi za Serikali wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB lililofanyika Kibaha mkoani Pwani.
Baadhi ya wafanyakazi wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia mada kwenye kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB kilichokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo kilichofanyika leo Kibaha mkoani Pwani
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bodi hiyo pamoja na wageni waalikwa wakati wa wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa PSPTB likilokuwa na lengo la kutathimini Utendaji kazi wa Bodi hiyo lililofanyika leo Kibaha mkoani Pwani.
Kikao kikiendelea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...