*Mkurugenzi Mtendaji aelezea walivyojipanga kukabili na mgao wa umeme, sasa mambo safi

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO)limetoa taarifa ya hali ya upatikanaji umeme nchini ambayo umeendelea kuimarika huku likitumia nafasi hiyo kueleza namna ambavyo limejipanga kusimamia Sera yake ya mazingira kwa lengo la kuhamasisha wanannchi kutunza mazingira sambamba na vyanzo vya maji.

Katika kusimamia Sera hiyo pamoja na mambo mengine TANESCO wako kwenye hatua ya kufikiria kuwa na tukio kama kama la tamasha ambalo litahusika kufanya shughuli mbalimbali za kimazingira na tamasha hilo litakuwa likifanyika kila mwaka lengo kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa kupanda miti na kutunza vyanzo vya maji ili kulinda mabwawa yanayotumika kuzalisha umeme.

Akizungumza leo Januari 31,2023 jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji umeme nchini ambayo imeendelea kuimarika, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Maharage Chande amesema wanatambua umuhimu wa kuwepo kwa vyanzo vya maji na mazingira na bahati nzuri wao Sera yao ni  mazingira.

Chande amesema kupitia Sera ya mazingira wamekuwa wakihakikisha wanashiriki kikamilifu katika utunzaji wa  misitu na kuhakikisha wanashughulika na shughuli mbalimbali za kuleta chachu kwa wananchi kujua umuhimu wa kutunza mazingira

Pia amesema katika upande wa Menejimenti  ya TANESCO wametangaza ajira hivi karibuni na wanatarajia kuajiri mtalaamu wa mazingira ambaye yeye atahusika katika kusimamia eneo hilo kwa kushirikiana walioko sasa.

"Pia TANESCO ni wachangiaji wakubwa katika mifuko ya mabonde kwa maana ya fedha kila mwaka tunalipa tozo kwenye mifuko ya mabonde ambayo fedha hizo moja ya kazi yake ni kusaidia kazi za kulinda vyanzo,"amesema Chande na kuongeza kama Menejimenti wanafikiria kuanzisha tukio kubwa la mazingira ambalo litakuwa linaleta chachu kwa wananchi kupenda kupanda miti na kutunza mazingira.

Ameongeza kwamba wanataka watu wawe wanafikiria kila mwaka kama ilivyo tamasha la  Fiesta, kwa mfano wanakwenda Rufiji na kisha wanapanda miti na kuhamasisha kutunza vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.Kwa hiyo kama menejiment tuko kwenye hatua ya kuweka  Idea kwa ajili ya kufanikisha jambo hilo na tutakapokuwa tayari tutashikisha vyombo vya habari kwa ajili ya kuhamasisha.

"Kama mtoto mdogo anavyojua muziki ndivyo tunavyotka ajue na mazingira kwasababu mabadiliko ya tabianchi yako na kwenye mazingira huo ndio mpango Wetu maana sera yetu TANESCO ni mazingira."

Awali Mkurugenzi huyo alipokuwa anazungumzia hali ya upatikanaji umeme nchini amesema mwaka jana kulikuwa na upungufu wa umeme wa kati ya megawati 200 hadi megawati 300 za umeme na hivyo Shirika lilitoa taarifa ya mipango ya kukabillana na hali hiyo kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu

"Tunapenda kutoa taarifa upungufu huo umepungua kwa klasi kikubwa na Kufanya hali ya upatikanaji wa umeme kuboreka zaidi, hii inatokana na mipango ya muda mfupl na wa kati ambayo imekwishatekelezwa."

Ametaja mipango ya muda mfupi iliyokamilika ni kwamba tayari wameshakamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kinyerezi namba ll na umesnaanza kuzalisha megawati 45 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzla Novemba 24, 2022.

Wamekamilisha matengenezo ya mtambo miwili iliyopo katika kituo cha Ubungo namba na

imeshaanza kuzalisha kati ya megawati 35 na 40 za umeme kwenye Gridi ya Taita kuanzia Novemba  25,  2022.Aidha wamekamilisha matengenezo ya mtambo mmoja wa kituo cha Kidatu na umeshaanza kuzalisha megawati 50 za umeme kwenye Gridi ya Taifa kuanzia tarehe 30 Novemba 2022.

Pia wamekamilisha ufungaji wa mitambo mitatu iliyopo katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba (Kinyerezi l Extension) na inaingiza megawati 120 za umeme kwenye Gridi ya Taita.

Kuhusu mipango ya muda wa kati, Chande amesema inaendelea na hivi karibuni majaribio ya mtambo mmoja uliopo katika kituo cha Ubungo namba l yanatarajiwa kukamilika ikapo mwishoni mwa  Februari 2023.

Pia amesema wanategemea mtambo wa mwisho uliopo katika kituo cha upanuzi cha Kinyerezi namba Kinyerezi Extension) utaanza kuzalisha megawati 45 za umeme kwenye Gridi ya Taifa ifikapomwishoni mwa mwezi Februari 2023.

"Licha ya kwamba hali a upatikanaji umeme imeboreka, Shirika limeendelea kushuhudia ongezeko kubwa la matumizi ya umeme kutoka asilimia 6 hadi 11 kwa mwaka, ongezeko hili limeshuhudiwa katika kipindi cha miaka miwill kutokana na ukuaji wa shughul za kiuchumi. Vilevile, mvua za vuli zilizonyesha hivi karibuni hazikuwa toshelevu kama ilivyotegemwa.

"Aidha, Shirika litaendelea kufanya matengenezo ya mitambo yake ambayo haikufanyiwa matengenezo kwa muda mrefu palenafasi inapopatikana na tutawajulisha wateja kuwa yanafanyika.Hali hii izidi kuboreka na iwe  ya kudumu, Shirika linaendelea na ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (ONHPP) ambalo limefikia asilimia 80.22 hadi kufikia Desemba 31, 2022."

Chande ameongeza kwamba  urefu wa kina cha maji la bwawa hilo ukiwa umefikia mita 126.12 kutoka usawa wa bahari pamoja na kuanzisha miradi ya vituo vipya vya kutumia gesi na umeme jadidifu na matarajio yao iwapo mvua za zitanyesha vizuri ndani ya miezi 18 Bwawa hilo litakuwa limekamilika na kuanza majaribio ya kuzalisha umeme.

Alipoulizwa iwapo kama mgao umekwisha Kwa Sasa kutokana na mipango mbalimbali inayotekelezwa na Shirika hilo,amesema ni mapema sana kueleza kama mgao umekwisha maana hali ya mvua pamoja na miundombinu bado haijawa kwenye kutoa asilimia 100 kwamba mgao hakuna ,hivyo utakapofika wakati muafaka na wakajiridhisha kwamba hakuna tena mgao watatoa taarifa.

"Siwezi kusema kwamba hakuna tena mgao, ni kweli tangu Novemba, Desemba na Januari hatukuwa na changamoto kubwa ya umeme hivyo umekuwepo lakini siwezi kutoa uhakika hapa halafu kesho kukawa na mgao mkasema Chande muongo."




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...