Na Sultani Kipingo wa Michuzi TV


Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Slovakia nchini Tanzania Mhe. Moustafa  Khataw ametoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa za kiuchumi kwa kushirikiana na wenzao wa nchi hiyo ambao wameonesha nia ya dhati ya kutaka  kuwekeza Pamoja  kufanya biashara na Tanzania.

 

Mhe. Khataw ameyasema hayo katika mahojiano maalumu wakati wa kongamano la uwekezaji na biashara la Umoja wa Nchi za Ulaya lililofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

 

Amesema Slovakia, iliyojipatia uhuru wake Januari 1, 1993 baada ya kuvunjika kwa amani umoja wake na Czechoslovakia, ni nchi iliyoendelea na yenye uchumi wa hali ya juu wa kipato, ikishika nafasi ya 45 katika Kielelezo cha Maendeleo ya Kibinadamu.

 

Mhe. Khatawa amesema jumla ya makampuni 18 toka Slovakia  yamehudhuria kongamano hilo la biashara la EU lililofunguliwa siku ya Alhamisi na Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango na kufungwa siku ya Ijumaa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

 

Pamoja na mambo mengine, amesema makampuni kadhaa yamedhamiria kuwekeza nchini Tanzania katika Nyanja mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa nyumba bora za bei nafuu na uzalishaji wa mbolea halisi.

 

Amesema Slovakia pia ni wazalishaji wakuu wa magari kwa kila mtu duniani, ambapo ilitengeneza jumla ya magari milioni 1.1 mwaka wa 2019, ikiwa ni asilimia 43 ya jumla ya pato lake la kiviwanda. 

 

“Kuvurugika kwa uchumi katika maeneo yao kutokana na mgogoro wa Urusi na Ukraine wenzetu hawa wa Slovakia wameamua kugeukia Afrika kuendeleza shughuli zao za biashara na uzalishaji na wamevutiwa mno na Tanzania kwa kuwa nchi ya amani na vivutio vyema vya uwekezaji”, alisema Mhe. Khataw.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...