Na Humphrey shao Michuzi Tv.

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimezindua klabu ya ujasiriamali kwa shule ya sekondari Temeke Wailes iliyoko Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi wa klabu hiyo ulifanyika kwenye shule hiyo

Chuo hicho kimesema vilabu hivyo vinalenga kuwawezesha wanafunzi kukua wakifahamu masuala mbalimbali ya biashara tangu utotoni ili waweze kuwa wajasiriamali siku za mbele.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa klabu hiyo Mkurugenzi wa Shahada za Juu, Tafiti na Ushauri wa chuo hicho, Dk. Tumaini Ubadius, alisema wanalenga kuzifikia shule zote za Dar es Salaam.

Dk. Tumaini amesema chuo hicho kimeona ni muhimu wanafunzi wakaanza kufundishwa kuhusu ujasiriamali wakiwa wadogo ili wanapohitimu elimu ya juu wawe na uelewa mpana kuhusu masuala ya biashara.

CBE ina kampasi zake kama Mbeya, Mwanza, Dodoma na Zanzibar.

Mkuu wa shule hiyo, Catherine Mdachi aliushukuru uongozi wa CBE kwa kuichagua shule hiyo kuwa miongoni mwa shule za mwanzo kuwa na klabu hiyo.

“Kuna mkuu wa shule moja alinipigia simu kuniambia hivi kwanini hao CBE wameamua kuja huko na kuja huko kwenu nikawaambia ni habati yetu,” amesema

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutujengea madarasa ili watoto wetu wapate sehemu ya kusoma, Huku Temeke hatujui nyota ya kijani tuna watoto wengi lakini tunamshukuru mama ametujengea madarasa mengi,”

Alisema uamuzi huo wa CBE umekuja wakati muafaka kwasababu kuna tatizo kubwa la ajira kwa hiyo kuwafundisha wanafunzi ujasiriamali kutawasaidia kujiajiri kwa kuanzisha biashara zao.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Wailes iliyoko Temeke jijini Dar es Salam wakionyesha utaalamu waoa wa kutengeneza sabuni shuleni hapo mbele ya viongozi kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), walipoenda shuleni hapo kufungua klabau ya ujasiriamali.
Mkurugenzi wa Shahada za Juu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Utafiti na Ushuri (CBE) Dk. Tumaini Ubadius, akimlisha keki mmoja wa wanafunzi wa shule ya Temeke Wailes jijini Dar es Salaam wakati walipozindua klabu ya ujasiriamali shuleni hapo
Mwalimu Mkuu wa shule ya Temeke Wailes, Catherine Mdachi na Mkurugenzi wa Shahada za Juu, Utafiti na Ushauri wa  wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),dk. Tumaini Ubadius, wakikata keki kuashiria uzinduzi wa klabu ya ujasiriamali shuleni hapo mwishoni mwa wiki
Wanafunzi wa shule ya sekondari Temeke Wailes jijini Dar es Salam wakiimbia wimbo wa taifa kabla ya uzinduzi wa klabu ya ujasiriamali iliyozinduliwa shuleni hapo mwishoni mwa wiki na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...