
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa Daud Yassin katikati akisikiliza maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa juu ya utekelezaji wa miradi ya Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa Daud Yassin katikati akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego Iringa juu ya utekelezaji wa miradi ya iliyoainishwa kwenye Ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi

Na Fredy Mgunda, Iringa.
CHAMA cha mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimewataka watendaji kutekeleza miradi yote kwa uadilifu mkubwa ili wananchi waendelee kukiamilini chama hicho kila Kona.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkoa wa Iringa mwenyekiti wa chama hicho, Daud Yassin Alisema kuwa
Kilichobaki ni kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na kumuunga mkono Rais Samia
Yassin amesema Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Iringa imekagua Utekekezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kuridhishwa na miradi waliyopitia.
Aidha Yassin amewataka watendaji kufanya kazi kwa uadilifu katika kuwatumikia wananchi badala ya kuwasubirisha kwa yake yanayowezekana kufanyika.
Akizungumza wakati akihitimisha ziara hiyo baada ya kukagua miradi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Yasin alisema ili kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan lazima watendaji wafanye kazi kwa bidii na weledi.
"Linalowezekana leo lisingoje kesho, kama Mwananchi amekuja kupata huduma na unaweza kumsaidia leo usimwambie aje kesho, mara njoo jumatatu, haipendezi," amesema Yasin na kuongeza;
"Kamati ya Siasa wamekagua miradi na wamesema wameridhishwa vinginevyo wangesema."
Alisema Rais Dkt Samia ametoa fedha nyingi kwa ajili ya utekekezaji wa miradi mbalimba. hivyo ujenzi wa miradi hiyo lazima uendane na fedha zilizotolewa.
"Rais wetu anafanya kazi kubwa sana lazima tumuunge mkono," alisema.
Kamati hiyo ilipitia miradi mbalimbali katika Wilaya za Mufindi, Kilolo na Iringa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...