Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya pamoja na Sekta Binafsi ya Tanzania imeandaa Kongamano la Biashara kati ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Ulaya linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 23 hadi 24 Februari, 2023 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Julius Nyerere International Conference Centre) uliopo jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo linatarajiwa kujumuisha zaidi ya washiriki 600 kutoka nchi za Umoja wa Ulaya na Tanzania linalenga kuwaunganisha washiriki hao ili kuwawezesha kubadilishana uzoefu, kushirikiana na watoa maamuzi na kukutana na wawekezaji wanaofaa pamoja na kujenga uelewa kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo kwa sekta ya umma na binafsi ambapo, Hati za Makubaliano mbalimbali ya Uwekezaji baina ya Tanzania na Nchi za Umoja wa Ulaya zitatiwa saini.

Kongamano hilo linatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, akimwakilisha Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na litafungwa rasmi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi ambaye atashuhudia utiaji saini wa mikataba ya fedha na hati za makubaliano.

Aidha, Kongamano hili litahudhuriwa na Mawaziri nane (8) kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mabalozi sita (6) wa Tanzania katika nchi za Umoja wa Ulaya ambao watashiriki katika vikao vya majadiliano kati ya Serikali na Biashara.

Hivyo ninatarajia kuona Kongamano hili la Biashara la kwanza kuwa fursa ya kuvutia wawekezaji, teknolojia na utalaamu katika nchi yetu na kuvutia biashara na uwekezaji kutoka duniani kote katika sekta za nishati, madini na kilimo endelevu. Hivyo tunatarajia hati za makubaliano zitakazotiwa saini zitaendeleza na kukuza biashara kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya, zitaongeza ajira kwa vijana na zitachangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu

Aidha, Wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania mtumie fursa hii vizuri kuendeleza na kukuza biashara yenu kwa kujifunza mbinu mpya za kibiashara, kupata wabia na masoko ya bidhaa zetu nje ya nchi.
Waziri wa Uwekezaji, Biashara na Viwanda, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji( katikati) akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuhusu kongamano la uwekezaji la Umoja wa nchi za Ulaya(EU Tanzania business forum 2023) linalotarajiwa kufanyika alhamisi na ijumaa wiki ijayo, linalolenga kuwaunganisha wawekezaji wa nje na wafanyabiashara wa ndani ya ujumla wao 600 kwa kubadilishana uzoefu na kushirkiana na watoa maamuzi. Wengine kushoto ni Naibu mkuu wa shughuli za ubalozi kutoka ubalozi wa Ufaransa nchini, Axel-David Guillon, Naibu Balozi wa EU nchini, Emilio Rossetti, wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wizara ya Uwekezaji, Ally Gugu na kulia ni Kinanasy Seif kutoka TPSF
Kinanasy Seif kutoka TPSF akizungumza na waandishi wa habari na wadau waliohudhuria kwenye mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...