MKUU wa Mkoa wa Pwani ,alhaj Abubakar Kunenge amewataka Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutembea kifua mbele ,kutokana na utekelezaji mkubwa wa kimaendeleo unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan .
Kunenge aliyasema hayo ,wakati Mwenyekiti wa UWT Taifa Mery Chatanda alipofika ofisini kwake, katika kikao kazi.
Alisema ,hiki ni kipindi cha kutamba kutokana na utendaji wa hali ya juu unaofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na amekuwa kiongozi wa pekee mwenye ushawishi duniani.
Aidha aliwapongeza viongozi wa UWT Mkoa wa Pwani kwa ushirikiano mkubwa wanaoipatia Serikali ya mkoa katika utekelezaji wa majukumu yake .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Taifa ,Mery Chatanda alimpongeza Mkuu wa Mkoa kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa katika chama na hii ndio sahihi katika utendaji shirikishi kati ya Chama na Serikali .
Amemtaka Mkuu huyo wa Mkoa, kuendelea kuwa miongoni mwa watekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa usimamizi uliotukuka kwenye miradi ya maendeleo ya jamii ili kukuza uchumi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...