Na Chalila Kibuda, Michuzi TV , Bahi

MKUU wa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma  Godwin Gondwe  ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Bahi .


Akizungumza kwenye ziara iliyofanyika  Februari 15 , 2023, Gondwe amesema uwepo wa chuo hicho utaleta chachu ya mabadiliko ya kiuchumi wilayani hapo kwani wananchi watapata ujuzi utakaoongeza thamani katika shughuli zao na kuongeza mapato.


“Tunaamini kabisa ujuzi utakaotolewa hapa utawasaidia wanaBahi kuongeza uzalishaji katika shughuli za kilimo, ufugaji na nyingine na hivyo kuleta tija zaidi,”amesema Gondwe huku akiishauri VETA kuandaa programu za mafunzo kwa kuzingatia zaidi shughuli za kiuchumi za wananchi wa Wilaya hiyo ambazo ni ufugaji, kilimo na madini.


Aidha Gondwe ameitaka VETA kutoa kipaumbele kwenye michezo kwa kutenga maeneo ya wanafunzi kufanya michezo mbalimbali ili kukuza umoja, mshikamano na vipaji wa vijana.


Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma Stanslaus Ntibara amesema ujenzi wa chuo hicho umefikia asilimia 90.


Chuo cha VETA cha Wilaya ya Bahi ni miongoni mwa vyuo vipya 25 vya Wilaya nchini ambapo chuo hicho kinajengwa na kusimamiwa na chuo cha VETA Dodoma kwa kutumia nguvu za ndani (Force Account).


 Ntibara ametaja kozi zitakazotolewa katika chuo hicho kwa awamu ya kwanza kuwa ni Uhazili na Kompyuta,Ushonaji, Uashi,Ufundi Umeme,Ufundi Magari na Uchomeleaji Vyuma.


Chuo hicho kitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi 300 kwa kozi za muda mrefu na 400 kwa kozi za muda mfupi ambapo nafasi za bweni ni kwa wanafunzi 144.Mkuu wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe akuzungumza wakati alipotembelea Chuo cha VETA Bahi kuangalia hatua xa ujenzi ulipofikia.Mkuu wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe akuzungumza wakati alipotembelea Chuo cha VETA Bahi kuangalia hatua xa ujenzi ulipofikia

Baadhi ya Picha ya Ujenzi wa Chuo cha VETA wakati Mkuu wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe akikagua ujenzi wa Chuo hicho.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...