MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga Husna Sekiboko amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Tanga.
Sekiboko ametoa shukrani hizo wakati wa ziara yake ya tarafa kwa tarafa yenye lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua pamoja na kukagua miradi ya maendeleo.
Amesema Rais Samia amekusudia kuleta maendeleo kwa wananchi, hivyo ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi wote bila kujali vyama waendelee kumuunga mkono ili aweze kutimiza lengo lake la kuleta maendeleo katika nyanja zote.
" Rais Samia tunakushukuru kwa kuendelea kutuletea maendeleo sisi wananchi wako na haya mambo mkubwa anayofanya Mama yetu ni lazima wananchi watamuunga mkono na kumchagua ili aendelee kuongoza katika awamu ijayo."
Katika hatua nyingine Mbunge huyo amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawekeza katika elimu ya awali na msingi ili kuwajengea uwezo watoto wao ambao ni Taifa la kesho.
Amesisitiza kila mzazi anajukumu la kumuandikisha mtoto wake ili aweze kupata haki yake ya elimu ambayo alisema Serikali ya awamu ya sita imekuwa ikitoa elimu bila malipo.
Aidha Mbunge huyo wa Viti Maalum Mkoa wa Tanga ameanza ziara rasmi ya tarafa mwa Tarafa kwa kuanza na Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga huku akitarajia kupita katika tarafa zote zilizopo kwenye Mkoa waTanga
Katika ziara hiyo Sekiboko ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Elimu ,Utamaduni na Michezo ameambatana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali ambapo wameweza kukutana na makundi yote pamoja na kufanya nkutano wa hadhara.
Hata hivyo wananchi wa Tarafa hiyo wamemshukuru Rais Samia Kwa kuendelea kuwapatia fedha nyingi za miradi ya maendeleo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...