NA Yeremias Ngerangera…Namtumbo
MJASILIAMALI Deogratias Vicent Gwasa shabiki wa timu ya Yanga wa kijiji cha Ligunga kata ya Lusewa wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma alikutwa na umauti kwenye kibanda umiza mara baada ya Timu yake ya Yanga kuambulia kipigo cha goli mbili na timu ya US Monastir huko Tunisia hapo jana.

Kwa mujibu wa shemeji ya marehemu Sadath Ngeleka alisema chanzo cha marehemu kukutwa na umauti ni mshituko wa matokeo ya timu yake ya Yanga baada ya kupokea kipigo kutoka kwa timu ya Us monastir kule Tunisia.

Ngeleka alidai marehemu toka asubuhi siku ya jumapili alikuwa na afya njema ,kwani aliweza kuhudhuria misa takatifu kanisani kijijini hapo na kisha kuendelea na kazi zake za biashara mpaka ilipofika muda wa saa moja usiku alielekea kwenye kibanda umiza kwa mwalimu Donatus Kapinga kuangalia mechi kati ya timu yake ya Yanga na Us Monastir

Matokeo ya Timu ya Yanga kufungwa magoli mawili yaliibua shangwe,vifijo na nderemo kwa mashabiki wa timu ya simba hali iliyomfanya Deogratias Vicent Gwasa aishiwe nguvu na kudondoka akiwa ukumbini humo na kukimbizwa zahanati ya ligunga na baada ya muda mfupi alipoteza maisha

Rajabu Sangana mwenyekiti wa tawi la Yanga kata ya Lusewa alikiri kumpoteza mwanachama wa Yanga katika tawi lake kwa sababu ya mshituko alioupata baada ya timu yake ya Yanga kufungwa goli mbili na US monastir

Marehemu Deogratias Gwasa alizikwa jana siku ya jumatatu kijijini kwao Ligunga kata ya Lusewa ambapo ameacha mke na watoto wawili.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...