JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dar ea Salaam imeunda Kamati ndogo za Jumuiya hiyo ili kuweza kuhakikisha Jumuiya ya Wazazi ya mkoa huo inakuwa dira ya mkoa na inayokwenda kusimamiwa na kuhakikisha inatekeleza na kusimamia mipango kazi ambayo wamejiwekea kwa miaka mitano.
Akizungumza
katika hafla ya kuwakabidhi barua za uteuzi Wanakamati, leo Februri 25,
2023 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM) Mkoa
Dar ea Salaam, Bi. Khadija Ally Said amesema anategemea ushirikiano
mkubwa kutoka kwenye Kamati zilizoundwa na kuhakikisha kazi za Jumuiya
ya wazazi ndani ya mkoa wa Dar es salaam zinafanyika vizuri.
Kamati
ambazo zimeundwa na kutangazwa ni Kamati tano ambazo ni Kamati ya
Miradi, Uchumi na Maendeleo, Kamati ya Utamaduni, Michezo na Mazingira,
Kamati ya Elimu, Afya na Malezi, Kamati ya Nidhamu na Maadili pamoja na
Kamati ya Habari za Jumuiya.
Kuhusu
Kamati ya Elimu, Afya na Malezi, Bi. Khadija amesema wao kama Jumuiya
ya Wazazi, malezi ni ajenda yao kitaifa, ndiyo maana wanakuja na
Kaulimbiu ya ‘Malezi bora kwa Mtoto’, Faraja ya Kesho ya Mzazi na
Taifa’, ambapo Kamati hiyo ina Wataalamu ambao wataenda kufanya mafunzo
kwa viongozi wa ngazi ya kata, pia Kamati hiyo ina viongozi wa kiroho.
"Kamati
hii inaenda kusimamia mambo ya msingi sana ya malezi na maadili lakini
pia suala zima la elimu kuhakikisha ufaulu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa
Watoto wa Shule za Msingi na Sekondari unaongezeka, lakini tunaenda
kuanzisha Shule za awali ambayo kupitia hii Kamati wataweza kutuanzishia
umuhimu wa Shule za awali katika ngazi ya Kata, Wilaya lakini
kuhakikisha kwamba jumuiya ya wazazi inasimamia Elimu katika ubora wake
na afya vilevile,” amesema Bi. Khadija
Aidha,
Bi. Khadija amesema Kamati ya Miradi, Uchumi na Maendeleo inaenda
kusaidia kwa kiwango kikubwa ndani ya mkoa kwani katika sera za Siasa na
Uchumi lazima kuwe na Miradi ambayo iko katika hali sahihi na watafanya
kazi katika miradi ambayo Jumuiya ya Wazazi itaweza kubuni.
Pia
amesema kusimamia na kuiongoza kuhakikisha wanabadilisha hali ya
wanajumuiya wake katika ngazi ya Kata, Wilaya na Mkoa lakini pia kufanya
miradi ambayo inapeleka jumuiya na Chama cha Mapinduzi moja kwa moja na
wananchi katika kuongeza kipato chao.
Pamoja
na hayo, miongoni mwa Kamati ambazo zimeundwa, kuhusu Kamati ya
Utamduni, Michezo na Mazingira, amesema kuwa katika kujenga mahusiano
yetu lazima tuingie kwenye michezo, kwahiyo watakuwa na timu za wazazi
katika kata zao, watakuwa na mashindano ya michezo mbalimbali katika
kata, wilaya na katika ngazi ya mkoa.
"Tunategemea
kama tukifanya vizuri kuingia na kwenda hata nje ya nchi kupitia timu
zetu , na hii ni kwaajili ya kupanua wigo wa mahusiano kati ya Chama
lakini pia na wananchi wake kwahiyo michezo ndio sehemu peke yake watu
wanakutana kwa pamoja",
"Na
sisi jumuiya ya wazazi tutafanya kazi na mtu yoyote mwenye nia njema na
Tanzania, hasa katika kuhakikisha malezi ya watoto na vijana wetu
yanapewa kipaumbele. Ndio maana kamati hizi zimejumuisha makundi
mbalimbali ya kijamii, sio kamati za kishabiki." amesema Bi. Khadija
Kwa
upande wake, Mjumbe wa Kamati ya ya Elimu, Afya na Malezi, Bw. Ismail
Sadick (Suma Lee) amesema atajitahidi kushirikiana na wajumbe wengine
kuhakikisha suala la elimu na malezi linakuwa bora katika Mkoa wa Dar es
Salaam kwasababu katika Kamati hiyo wapo viongozi wa kiimani ambao pia
ataenda kushirikiana nao
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Khadija Ally Said akimkabidhi barua Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alhad ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Malezi kwenye Jumuiya hiyo wakati wa hafla fupi iliofanyika leo jijini Dar es salaam.
JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Dar ea Salaam imeunda Kamati ndogo za Jumuiya hiyo ili kuhakikisha Jumuiya hiyo inakuwa dira ya mkoa na inayokwenda kusimamiwa ndani ya miaka mitano kuhakikisha inatekeleza mipango kazi ambayo imejiwekea. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es
Salaam, Khadija Ally Said akimkabidhi barua Ndugu Mjumbe wa Kamati ya ya
Elimu, Afya na Malezi Bw.Ismail Sadick (Suma Lee) kwenye Jumuiya hiyo
wakati wa hafla fupi iliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es
Salaam, Khadija Ally Said akimkabidhi barua Ndugu David Minja ya kuwa
Mwenyekiti wa kamati ya uchumi wa Jumuiya hiyo wakati wa hafla fupi
iliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es
Salaam, Khadija Ally Said akizungumza wakati Jumuiya hiyo kukamilisha
kuunda Kamati ndogo za Jumuiya hiyo ili kuhakikisha inakuwa dira ya
mkoa na inayokwenda kusimamiwa ndani ya miaka mitano katika
kutekeleza na kusimamia mipango kazi ambayo imejiwekea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...