Njombe

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe ambaye pia ni diwani wa kata ya Utalingolo Erasto Mpete,ameagiza viongozi wa kata ya Utalingolo kwenda kuanza kutekeleza sheria ya kulipa faini ya shilingi elfu 50,000/= kwa yeyote atakayebainika akitupa taka ndani ya kata hiyo.

Mpete ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi zoezi la usafi wa mazingira ndani ya kata uliofanywa na mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ikiwa lengo ni kuhimiza maswala ya usafi,huku pia wakijipanga kufanya vizuri kwenye kampeni ya afya na usafi wa mazingira kitaifa kwa kuwa vijiji viwili ndani ya kata hiyo vimeingizwa katika kampeni hizo kitaifa.

Akizindua zoezi hilo mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ametoa wito kwa jamii wilayani humo kuhimizana katika usafi wa mazingira pamoja na usafi binafsi ili kukabiliana na magonjwa mbali mbali yakiwemo ya mlipuko.

"Huku kwetu ni baridi sana,tuhimizane watu kuoga ili hata tunapohudumia wageni tuwe wasafi maana unaweza ukaona wengine wanaoga asubuhi lakini ikifika jioni ukaona mmh! ukapiga deshi"amesema Kissa Kasongwa.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...