Na Kassim Nyaki, NCAA

Mabalozi 18 wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania wametembelea eneo la hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kufanya utalii katika vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika hifadhi hiyo

Kiongozi wa Mabalozi hao, Balozi Sandro De Olivera kutoka Nchi ya Angola ameeleza kuwa ujumbe wa mabalozi hao unajumuisha nchi za Namibia, Angola, Algeria, Msumbiji, Kenya, Somalia, Malawi, Saharawi, Namibia, Uganda, Sudan Kusini, Malawi, Nigeria na Uganda.

Balozi Olivera amebainisha kuwa wamekuwa wakisikia Utajiri wa vivutio mbalimbali vilivyoko Tanzania na kuamua kufanya Safari ya kitalii kushuhudia vivutio hivyo na kuwa Mabalozi wa vivutio hivyo wanaporudi kwenye nchi wanazoziwakilisha.

"Kuona ni Kuamini na tunaona Ngorongoro ina utajiri wa vivutio vya kila aina, ni eneo muhimu kwa mtu yoyote kutembelea na kuona" ameongeza Balozi Olivera

Naibu Kamishna wa Uhifadhi NCAA Needpeace Wambuya ameueleza ujumbe huo kuwa ujio wao ni sehemu ya kukuza mahusiano ya Kidiplomasia kupitia Sekta ya Utalii ambapo Tanzania imeendelea kutangaza vivutio vyake kwa wadau mbalimbali hali inayochangia kuendelea kupokea makundi ya wageni ikiwepo Viongozi wa mataifa mbalimbali.

Mkuu wa Huduma za Utalii NCAA Peter Makutian ameeleza ujumbe huo kuwa Ngorongoro ni eneo lenye vivutio mbalimbali ikiwemo wanyama maarufu watano (Tembo, Simba, Faru, Chui na Nyati), Kreta za aina tatu, vivutio vya malikale ambavyo ni sehemu ya urithi wa dunia, Milima na mandhari asilia yaliyohifadhiwa kwa mda mrefu.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...