Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya hewa Nchini, (TMA) akizungumza na waandishi wa habari wakati akisoma Utabiri wa mvua msimu wa Masika (Machi hadi Mei 20023) jijini Dar es Salaam leo Februari 22,2023. Kulia kwake ni Dkt. mafuru Kantamla Kaimu Meneja Kituo Kikuu Cha Utabiri TMA.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAMLAKA ya hali ya hewa nchini (TMA) imesema katika msimu wa mvua za masika mwaka huu takribani mikoa 11,inatarajia kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani huku mikoa minne ikitarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Mikoa hiyo 11 inayotarajiwa kupata mvua wastani hadi chini ya wastani ni pamoja na Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga,Simiyu, Mara,Arusha Manyara, Kilimanjaro,Tanga pamoja Kisiwa cha Pemba huku maeneo machache ya Dar es Salaam, Pwani ikijumuisha Mafia, kaskazini mwa Morogoro pamoja na visiwa vya Unguja vikitarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi juu ya wastani.

Akizunguma wakati wa kutangaza Utabiri wa Mwenendo wa mvua za Masika, kipindi cha Mwezi Machi hadi Mei 2025 jijini Dar es Salaam leo Februari 22,2023 , Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Dkt. Ladislus Chang'a amesema msimu wa mvua za Masika a mahsusi kwa maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki,pwani ya kaskazini pamoja na kaskazini mwa mkoa wa kigoma.

Amesema kutokana na mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa katika kipindi cha msimu, mvua za wastani hadi juu ya wastani zitanyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (katika visiwa vya Mafia), Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro na Kisiwa cha unguja.

Amesema ongezeko la mvua katika maeneo hayo linatarajiwa kuanza mwezi Mei, 2023 hususani katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini.

"Mvua za Masika zinatarajiwa kuanza kunyesha mwezi Machi katika maeneo Mengi na zinatarajiwa kumalizika katikati ya wiki ya nne ya mwezi Mei 2023 huku muendelezo wa mvua za nje ya msimu ukitarajiwa mwezi J Juni 2023 katika maeneo machache ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini" amesema Dkt. Chang'a.

"Katika maeneo ya ukanda wa Ziwaa Victoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma mvua zinatarajia kuanza wiki ya kwanza na ya pili ya mwezi machi 2023 na kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Mei.

huku katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani katika visiwa vya Mafia, Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro na kisiwa cha unguja mvua zinatarajia kuanza wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Machi na kuisha Juni,2023.’’ Ameongeza.

Amesema katika mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro mvua iznatarajiwa kuanza kunyesha wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Machi 2023 na kumalizika wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei 2023,’’

Akizungumzia Athari zinazoweza kutokea Dkt. Chang'a amesema, mvua chache zenye mtawanyiko usioridhisha kwa maeneo yanatarajiwa kunyesha mvua za wastani hadi chini ya wastani, kunaweza kusababisha upungufu wa unyevu kwenye udongo na upatikanaji wa maji kwa shughuli za kilimo.

"Shughuli za kilimo zinatarajiwa kuendelea kama kawaida isipokuwa kwa baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kupata mvua chache zenye mtawanyiko hafifu yanaweza kukumbwa na upungufu wa unyevu wa udongo na upatikanaji wa maji kwa shughuli za kilimo" amesema.

Ameongeza kuwa, mvua za wastani hadi chini ya wastani zinazotarajiwa zinaweza kuathiri upatikanaji w maji safi na salama na hivyo inaweza kusababishi mgonjwa ya mlipuko.

Aidha amezishauri menejimenti za maafa kufuatilia kwa karibu taarifa za tahadhari na kushirikiana kuchukua hatua za kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa yanayoweza kujitokeza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...