Rai imetolewa kwa Wasanii hapa nchini kuhakikisha mikopo ya fedha waliyopewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan waitumie kwa tija iliyokusudiwa katika kujiletea maendeleo kwa Shabaha ya Kujiimarisha Kiuchumi ikiwa ni pamoja na kukuza tasnia ya Sanaa kwa Ujumla.


Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama wakati akizungumzia kuhusiana na maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2023 ambalo limepangwa kufanyika Jijini Dar es Salaam April 09.

"Kupitia mikopo hiyo, mfanyie mambo ya msingi, mtunge nyimbo nzuri na mambo mengine ya maendeleo ili mjiinue kiuchumi"

"Tunamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwani ana upendo wa hali ya juu, mwenye hofu ya Mungu, na mwenye upendo wa dhati kwa watanzania hasa kwa kuwakumbuka wasanii wote wa Tanzania kwa kuwapa mikopo" amesema Msama.

Mikopo hiyo ikiwa ni ya awamu ya pili kwa wasanii, Serikali ilitoa shilingi Milioni 850 kwa wasanii 40 nchini,  ambapo wasanii waliiomba kupitia wizara ya utamaduni, sanaa na michezo.

Msama pia amemshukuru, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Hassan Abas kwa kufanya kazi nzuri kwa upande wa tasnia ya sanaa ambapo amewataka wasanii kuunga mkono juhudi hizo za Serikali.

Kwa Upande wake Emmanuel Mabisa ambae ni Miongoni mwa Waratibu wa tamasha hilo la injili, amesema Maandalizi ya Tamasha la pasaka litakalofanyika Aprili 09 mwaka huu Jijini Dar es Salaam yapo vizuri,  ambapo kwa wiki ijayo wataanza kutangaza majina ya waimbaji watakaoimba katika tamasha hilo kutoka ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama wakati akizungumzia na Waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2023 ambalo limepangwa kufanyika Jijini Dar es Salaam April 09.
Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama akisisitiza jambo mbele ya Waandishi wa habari akigusia pia fedha walizopewa Wasanii na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwamba wazitumie kwa tija iliyokusudiwa katika kujiletea maendeleo kwa Shabaha ya Kujiimarisha Kiuchumi ikiwa ni pamoja na kukuza tasnia ya Sanaa kwa Ujumla,Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka Emmanuel Mabisa.
Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka (kushoto) Emmanuel Mabisa akieleza maandalizi ya Tamasha la Pasaka 2023 ambalo limepangwa kufanyika Jijini Dar es Salaam April 09.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...