Yatoa udhamini kwa wanafunzi waliofanya vizuri kidato cha Nne, yatangaza fursa Pre- Form Five


SHULE Ya Sekondari ya Wasichana ya John The Baptist imeeleza mikakati ya kuwahimiza watoto wakike kupenda masomo ya Sayansi hasa Hesabu na kuondokana na dhana ya ugumu wa masomo hayo. Akizungumza wakati wa kikao cha wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo yenye kidato kwanza hadi sita kilichofanyika katika viwanja vya shule hiyo leo jijini Dar es Salaam Mwalimu wa Taaluma wa John The Bapstist Nia Kadula amesema shule imeweka mipango madhubuti ikiwemo kuwa na programu za masomo ya ziada ili kuweza kuwa na wanasayansi wengi wa kike. "Wazazi tushirikiane katika hili, tuwape moyo watoto wetu kwa kuwasapoti hasa katika vifaa vya kujifunzia ili kuwajengea kujiamini na kuona wanaweza." Amesema. Ameeleza kuwa katika kuhakikisha suala hilo linafanikiwa wamekuwa wakishirikiana na walimu kutoka shule zinazofanya vizuri katika Mkoa wa Dar es Salaam ili kubadilishana uzoefu pamoja na maarifa. Pia ameeleza kuwa katika kutoa motisha kwa wanafunzi, shule imetoa udhamini wa ada (shilingi milioni moja) kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani yao ya kidato cha Nne 2022 na kuendelea na masomo ya kidato cha tano shuleni hapo Julai mwaka huu. Amesema wanashirikiana kwa ukaribu na Serikali kukuza elimu nchini na tayari wameanza kutoa elimu kwa ngazi awali huku mpango wa kutoa elimu kwa ngazi ya Msingi ukiwa tayari. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John The Bapstist Kaimu Mkuu wa Shule hiyo Samson Sixbert amesema katika kufikia malengo ushirikiano wa Shule, mzazi/ mlezi na mwanafunzi ni mhimili mkubwa. Taaluma, kuhusiana hilo ameeleza kuwa shule ina mkakati wa kutenga muda zaidi na kuvuna matokeo bora katika mitihani ya shule na Taifa. " Wazazi tushirikiane katika hili iki tuweza kuwawezesha vijana wetu kufaulu vyema, matokeo ya mitihani ya Taifa inaimarika kila mwaka... Tushirikiane ili kuboresha matokeo ya shule yetu." Amesema. Nidhamu, amesema uongozi wa shule unasimamia nidhamu na maadili katika ngazi zote za walimu, wafanyakazi wasio walimu kw kuwa nidhamu na maadili ni chachu ya mafanikio. " Tunasimamia nidhamu katika ngazi zote, tuna chombo cha nidhamu kwa wanafunzi kinachosimamiwa na wanafunzi wenyewe na wanaonyana kwa mienendo isiyofaa, Kuna uhusiano mkubwa kati ya nidhamu na mafanikio na tunaendelea kulisimamia hilo " Amesema. Kuhusiana na suala la Afya, amesema shule imekuwa ikizingatia suala la Afya ili kuhakikisha wanafunzi wote wanakuwa na afya bora ya mwili na akili. "Tumekuwa tukihakikisha kila mwanafunzi analala na kuamka salama kupitia matroni, tunashauri wazazi wenye watoto wasio na bima ya afya tukate bima za afya kupitia mgongo wa shule kwa gharama za 50,400 na wenye bima ziwasilishwe kwa matrons kwa muda wote wanakuwa shuleni " Ameeleza. Aidha amesema kuwa nafasi za kidato cha tano kwa michepuo ya HKL, HGE, PCB, ECA na CBG zinatolewa na kwa wanafunzi watakaofanya vizuri katika masomo ya kidato cha sita wanaweza kupata ufadhili wa masomo nje ya nchi kwa masomo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla. Hafla hiyo imekwenda sambamba na utoaji zawadi kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri zaidi. Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John The Baptist Samson Sixbert akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo amewahimiza wazazi kushirikiana ili kutimiza malengo ya juu katika ufaulu. Leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya kidato cha Nne 2022, na kupata udhamini wa ada katika masomo yao ya kidato cha tano wakifuatilia kikao hicho.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...