MCHEZAJI wa Pool wa timu ya TaifaAbdallah Hussein kutoka Klabu ya Snipers yenye makazi yake Mwenge Mpakani, Dar es Salaam, ameteuliwa na Chama cha Pool Taifa kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Duniayanayotarajiwa kufanyika nchini China, yajulikanayo kama“World Heyball Championships 2023”.

Uteuzi wa Hussein umekamilika leo Februari 16 baada yamchakato uliofanywa na viongozi wa chama hichoakibebwauwezo mkubwa alioonyesha katika mashindano kadhaayaliyopita pamoja na kuwa na hati ya kusafiria (Passport).

Mwenyekiti wa Chama cha Pool, Isaac Togocho, amesema Hussein ataambatana na kiongozi mmoja wa chama hichoambaye atamteua hivi punde.


Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi Machi 21 – 27,2023 kwa hatua ya awali ya kufuzu na Machi 28 ni sherehe zaufunguzi rasmi wa fainali zenyewe zitakazoanza siku inayofuatana kuhitimishwa Aprili 5,2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...