Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa akionyeshwa Michoro ya Ramani ya Ujenzi wa Ukumbi wa Kimataifa wa Michezo (Sports Arena) unatarajiwa eneo la Kawe karibu na uwanja wa Tanganyika packers Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 14,2023 mara baada ya kukabidhiwa eneo la hekari 12 litakazotumika kujenga Ukumbi wa Kimataifa wa Michezo (Sports Arena) Tanganyika packers Kawe Jijini Dar es salaam akisisitiza kuwa Mkandarasi ataanza ujenzi mapema mwezi Machi.

Na Khadija Seif, Michuzi TV 

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mohamed Mchengerwa amesema Watanzania wana kiu ya kuona ukumbi wa Kimataifa wa Michezo ( Sports Arena) inajengwa nchini huku akieleza kwamba tayari Wizara imepokea hekari 12 eneo la Kawe jijini Dar es salaam kwa ajili ya ukumbi huo.

Akizungumza leo  Februari 14, 2023, Waziri Mohamed Mchengerwa wakati akikabidhiwa hekari hizo 12 , amesema kuwa Sports Arena itakayojengwa Kawe utakuwa na uwezo wa  kubeba watu 16000 na hivyo kutoa nafasi pia ya Watanzania kushuhudia matamasha mbalimbali yatakayokuwa yakifanyika katika ukumbi huo.

Aidha, Waziri Mchengerwa ameeleza kwamba  dhamira ya Dkt. Samia Suluhu ni kuhakikisha sekta ya burudani na michezo zinakuwa sekta zinazokwenda kuchangia pato la Taifa.

"Watanzania wamekuwa wakihoji kuwa tayari Bajeti imepitishwa lakini hawaoni utekelezaji wa ujenzi wa ukumbi huo, lakini tuwatoe hofu kuwa sasa tunaenda kuandika historia nchini Tanzania kujengwa kwa ukumbi huo wa Kimataifa,” amesema Waziri Mchengerwa.

Pia ameeleza Arena hiyo inatarajiwa kukamilika kati ya Agosti na Oktoba mwaka huu na utakuwa moja ya ukumbi mkubwa barani Afrika kama ilivyo Arena kubwa ya nchini Senegal inayochukua watu 15000.

“Tulipotoka hatukuwa na mipango mizuri hivyo tulivyoingia na Wasaidizi  wetu tumehakikisha tunaenda kuongeza nguvu kubwa tutengeneze mipango yetu, tutengeneze michoro na hatua zote tumekwisha kuzikamilisha na tunatarajia mwezi Machi mwaka huu kumkabidhi Mkandarasi na ujenzi.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba Wizara itahakikisha inasimama kidete  hadi kukamilisha maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukamilisha ujenzi huo wa ukumbi wa Arena nchini Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...