Mkurugenzi Mkuu wa NTS Bosch, Amin Lakhani akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 14, 2023 wakati wa uziduzi wa kituo cha maonesho na mauzo kilichopo Kamata Kariakoo.
Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya NTS-Bosch, Manoj Thakkar akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Februari 14, 2023 wakati wa uziduzi wa kituo cha maonesho na mauzo kilichopo Kamata Kariakoo.
.


KAMPUNI ya NST-Bosch wazindua kituo cha Maonesho, mauzo na huduma kwa wateja katika eneo la Kamata Kariakoo jijini Dar es Salaam leo Februari 14, 2023.

Akizungumza wakati wa kutambulisha kituo hicho, Mkurugenzi Mkuu, Aman Lankani amesema kuwa wasambazaji wa vifaa vya Bosch ninakuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kwa sababu vifaa vyake vinarahisha utanyaji kazi wa binadamu.

Amesema kuwa vifaa mbalimbali vya Kampuni hiyo vinamsaidia mtumiaji kutokutumia nguvu wakati wa ufanyaji kazi pia vinatumia betri katika utumiaji.

Lankani amesema kuwa NTS Bosch vitatoa huduma kwa mteja pamoja na kuuza bidhaa zote za umeme na vifaa vyake ikiwa ni pamoja na zana za usanifu majengo, vifaa vya uselemala pamoja na vifaa vinavyotumika kwenye biashara mbalimbali. 

Akizungumzia katika utoaji huduma amesema kuwa watatoa mafunzo ya mfano kwa wanunuaji wa bidhaa hizo na kuonesha jinsi zinavyofanya kazi kwa urahisi kulingana na mtumiaji anavyohitaji. Pia amesema kuwa pale vifaa hivyo vikiharibika wanatoa huduma ya kutengeneza pamoja kukarabati.

Kwa Upande wa Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa kampuni ya NTS-Bosch, Manoj Thakkar amesema kituo hicho kitawapa wateja matengenezo ya haraka na ufanisi, kuhakikisha zana zao zina ubora wa hali ya juuu katika ufanyaji wa kazi kila wakati.

Amesema kuwa tasnia ya vifaa vya Bosch imekuwa kutoka sekta ya magari hadi sekta ya zana nguvu, hivyo wateja wameombwa kutumia kituo hicho katika kujipatia huduma na vifaa mbalimbali.

"Wewe ni mkandrasi mtaalamu wa kampuni au mpenda DIY, NTS-Bosch ina zanz unazozihitaji ili kufanya kazi kwa usahihi." Amesema Thakkar

Kwa Upande wa uwekezaji amesema kuwa kwa mwaka huu serikali imewawezesha kufanya biashara kwa kufuata sheria na kanuni za nchi hivyo imewawezesha kuwafkishia huduma wananchi kwa urahisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...