Njombe

Wanafunzi wa kike katika shule za sekondari wilayani Njombe wametakiwa kuwa na misimamo na kukataa vishawishi vyote kutoka kwa wanaume ili kujiepusha na vitendo vya ukatili vinavyoweza kukatisha ndoto zao.

Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi wilaya ya Njombe Beatrice Malekela wakati akizungumza na wanafunzi wa kike zaidi ya 800 wa shule ya sekondari Maguvani,Mukilima na Makambako Sekondari katika halmashauri ya mji wa Makambako,ambapo amewataka wasikubaliane na aina yoyote ya ushawishi hata kama kwa kupewa fedha.

"Jifunze kusema hapana,yaani hata huko mtaani ukikuta mtu amekuja na kuanza kukugusa gusa lazima utolee taarifa hicho ni kiashiria kwamba kuna kitu kinafuata"amesema Betreace Malekela

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Makambako Keneth Haule amewataka wanafunzi hao wa kike kuheshimu wazazi wao na kusikiliza maonyo wanayopewa kwani ni kwa manufaa yao.

Naye Kiongozi wa dawati la jinsia na watoto ambaye ni mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi wilaya ya kipolisi Makambako Jane Mwampashe amewataka wanafunzi hao kutoa kuwa waoga wa kutoa taarifa pindi wanapofanyiwa ukatili ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...