Na Mwamvua Mwinyi, Pwani

WAHAMIAJI haramu wawili raia wa Nigeria na Cameroon wamekamatwa Mapinga Kibosha, Mkoani Pwani kwa kosa la kuishi nchini kinyume cha sheria pamoja na kudaiwa kutakatishaji fedha bandia na hati za kusafiria ,hali ambayo ingeweza kusababisha athari kiuchumi.

Kufuatia tukio hilo Mwenyekiti wa kamati ya usalama, mkoa wa Pwani alhaj Abubakari Kunenge , alieleza hatomvumilia raia yeyote wa nje atakaetaka kuishi Mkoani humo kinyume na Utaratibu ambapo ameeleza wale wanaoishi bila kufuata sheria na kubainika watachukuliwa hatua.

Alieleza ,Mcameroon Bertrand Noubissie alikutwa na karatasi zilizoandaliwa kwa kwa ajili kuchapisha noti bandia za pesa,kemikali na kasiki la kutunzia fedha.

Wakati wa upekuzi mtuhumiwa Livingston Ese Onayomake raia wa Nigeria alikutwa na Jumla ya pasipoti 34 ambazo si za kwake, ambapo kati ya hizo pasipoti 32 ni za Nigeria na pasipoti mbili ni za Ghana .

"Alipohojiwa alidai kuwa alichukua pasipoti hizo kwa lengo la kuwatafutia viza ya Uturuki wahusika"

Kunenge alieleza kwamba ,mkoa huo sio eneo salama la uhalifu Wala kuingia kiholela,na vyombo vyote vya kiusalama vimejipanga.

Nae ofisa uhamiaji mkoa wa Pwani,Omary Hassan alieleza "Tarehe 9 mwezi huu tulipokea taarifa fiche kutoka kwa msiri wetu kwamba katika eneo la Mapinga,Kibosha kuna watu ambao uraia na mienendo yao inatia mashaka,,Tarehe 10 timu ya Maafisa Uhamiaji walifanikiwa kufika katika eneo husika na kutekeleza jukumu lao ambapo walikamata raia wawili wa Afrika Magharibi kutoka Mataifa ya Cameroon na Nigeria Sambamba na kuwafanyia upekuzi maungoni na kwenye makazi yao"

"Raia hawa wa kigeni walikuwa wakiishi nyumbani kwa bi.New Era Nyirembe mwanamke kabila Mjita ambae kwasasa ni marehemu na alikuwa mke wa mtuhumiwa Bertrand Noubissie raia wa Cameroon "alieleza Hassan.

Hassan alikiri matukio ya aina hiyo kutokea na sio mara ya kwanza.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...