Wafanyakazi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT),wakienelea kuzalisha vipuli vya plastiki kwaajili ya magari na bajaji.

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wameombwa kutoa elimu kwa kiwango cha kimataifa na shindani ili kuwawezasha wahitimu wa chuo hicho kufanya kazi katika nchi mbalimbali.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Machi, 15, 2023 baada ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, utamaduni na Michezo walipotembelea Taasisi hiyo kujionea jinsi mradi wa Kuleta Mapinduzi kwenye elimu ya ufundi Afrika Mashariki (EASTRIP) unaofadhiriwa na Benki ya Dunia unavyotekelezwa.

Ambapo kwa Upande wa DIT kampasi ya Dar es Salaam wamenzisha Kituo cha Umahiri wa Tehama cha Kikanda (RAFIC) na Kwa Kampasi ya Mwanza wataanzisha Kituo cha Kikanda cha Umahiri wa Teknolojia ya Ngozi (CELPAT).

Amesema kuwa hatua kubwa ambayo imefanyika DIT kuingia mkataba na chuo Kimoja cha nchini China ambapo wanachuo watakao soma katika taasisis hiyo kuweza kwenda kujifunza nchini China huku wachina kuja kujifunza nchini.

"Tungependa makampuni yanapotaka kuajiri yapiganie kupata wahitimu waliotoka katika taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam." Amesema Prof. Mkenda

Wakati huo huo Prof. Mkenda ameiomba DIT kuzalisha bidhaa mbalimbali kibiashara katika viwanda nje ya chuo kwa kampuni tanzu inayomilikiwa na Chuo.

Amesema kuwa na Kampuni tanzu kutatoa fursa kwa wafanyabiashara binafsi wanaotaka kuchukua ubunifu huo kwenda kuzalisha bidhaa hizo kibiashara ili kutengeneza faida.

Makumu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Elimu Utamaduni na Michezo, Husna Juma Sekiboko amesema kuna haja ya kuwaunga mkono katika eneo la uzalishaji wa vipuli vya Magari na Bajaji ili waweze kuongeza mapato yao ya ndani na mapato ya serikali ikiwa pamoja na kupiga hatua za kibajeti.

Pia amewapongeza wafanyakazi wa DIT na wanachuo ambao wanafanya ubunifu wa uchapishaji wa

Teknolojia ya 3D ambayo wanaifanya katika taasisi hiyo.

"Teknolojia hiyo ni mpya na inapatikana Tanzania DIT peke yake, ni teknolojia nzuri itasaidia kama nchi kusonga mbele kiteknolojia."

Husna ameziomba taasisi nyingine za elimu ziige mfano wa DIT ikiwa ni pamoja na kuendeleza teknolojia yetu nchini.

Pia amewaomba wadau mbalimbali waweze kuwaendeleza watoto wakike wanaosoma masomo ya sayansi, ubunifu na teknolojia kwa njia ya kuwapa ufadhiri na kuwahamasisha wazidi kuyapenda masomo ya Sayansi.

Pia amesema wataishauri serikali ili iweze kupeleka vitendea kazi hasa komputa katika shule ili wanafunzi waweze kujifunza masomo mbalimbali kwa vitendo.

Kwa Upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia (DIT), Mhandisi Dkt. Richard Masika amesema maelekezo ya kuzalisha vipuli vya aina mbalimbali kama vya Chuma na vya plastiki na pia kuhamisha kutoka kwenye eneo la Taasisi na kuweka katika eneo jingine kwaajili ya uzalishaji wa Kibiashara watayafanyia kazi.

"Hilo tutalifanyia kazi, na kulitekeleza kwa wakati." Amesema Mhandisi Dkt. Masika

Mhandisi Dkt. Masika amesema kuwa kuitwa DIT nidhamana yenye wajibu na majukumu, majukumu waliyonayo ni pamoja na kuzalisha kupika wahandisi wanasayansi pamoja na mafundi ambao wanaweza kusimama katika nafasi mbalimbali kwa umahiri na wakiwa na ujuzi wa kutosha ambapo wanaweza wakajiajiri na kutengeneza ajira.

Pia amewakaribisha jamii na Wazazi kutembelea DIT ili waweza kuona shughuli zinazoendelea za kufundisha za kutafiti pamoja na utoaji ushauri wa kitaalamu.

Katika ziara hiyo wanakamati hao wa bunge walitembelea maeneo ya kujifunzi na uzalishaji ikiwa pamoja na eneo la uzalisha wa vipuli vya magari, eneo la kubadilishia magari ya yanayotumia mafuta kwenda kwenye gesi, eneo la uchapishaji kwa teknolojia ya 3D pamoja na darasa la watoto wakike wanaosoma masomo ya Sayansi pamoja na kupata taarifa ya Mradi wa EASTRIP.
Baadhi ya wanakamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, utamaduni na Michezo walipotembelea DIT  Machi 16, 2023 kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa katika taasisi hiyo.
Wanakamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, utamaduni na Michezo wakipata maelezo jinsi ya mfumo wa gesi kwenye gari unavyofanya kazi walipotembelea DIT jijini Dar es Salaam Machi 16, 2023.
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Prof. Preksedis  Ndomba akifafanua jambo kwa Wanakamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, utamaduni na Michezo walipotembelea DIT jijini Dar es Salaam Machi 16, 2023.
Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Prof. Preksedis  Ndomba akielezea mradi wa Kuleta Mapinduzi kwenye elimu ya ufundi Afrika Mashariki (EASTRIP) unaofadhiriwa na Benki ya Dunia unavyotekelezwa kwa  Wanakamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, utamaduni na Michezo walipotembelea DIT Machi 16, 2023 jijini Dar es Salaam.
Kifaa za Kiteknolojia cha kuchapisha 3D kilichopo DIT.
Baadhi ya Wanakamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, utamaduni na Michezo wakiangalia wakipata maelezo kwenye Ktudio ya kiteknolojia iliyopo DIT.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa. Adolf Mkenda akiteta jambo na mmoja ya Wanakamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, utamaduni na Michezo walipotembele DIT jijini Dar es Salaam Machi 17, 2023.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...