Mkurugenzi wa ZEEA Mh. Juma Burhani,Mkurugenzi wa SMIDA Mh. Soud Said Ali na Mkurugenzi Mtendaji wa Equity bank (T) Bi. Isabela Maganga wakionesha umma nyaraka baada ya kusaini makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja leo katika ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Raisi,kazi,uchumi na uwekezaji mh. Mudrick Soraga.[

Benki ya Equity Tanzania imeingia makubaliano ya kufanya kazi na taasisi ya ZEEA pamoja na SMIDA za Zanzibar kwa lengo la kuhakikisha wanatoa mikopo nafuu kwa wajasiriamali wakubwa na wadogo na kuwapa elimu za kifedha kama sehemu ya mkakati wa benki kuhakikisha wanatoa huduma bora na gharama nafuu kwa kila Mtanzania.

Makubaliano haya yatasaidia katika suala zima la
kuongeza ajira kupitia nguzo ya ujasiliamali kwani wajasiliamali
watapata mitaji ya kutosha kukuza biashara zao sambamba na kuongeza
ubunifu. Ili kufikiwa matamanio haya, Benki ya Equity itakuwa na mengi
na mahususi ambayo ni pamoja na:-
Kutumia miundombinu ya kibenki katika kuwezesha utoaji wa mikopo ambayo imethibitika, hii ni pamoja na mifumo na rasilimali watu Kutumia uzoefu wa ufuatiliaji mikopo ili kuhakikisha kuwa pesa inayokopeshwa pasi na riba inarejeshwa kwa wakati na kulingana na vigezo na masharti yaliyokubaliwa Kutoa taarifa kwa vyombo wabia (ZEEA na SMIDA) juu ya ufanisi wa program hii kwa wakati.
Kutoa mikopo kwa wakati (ndani ya siku 14 za kazi) Kuendelea kutoa mikopo bila riba wakati wote program hii kwa wajasiriamali katika Nyanja zote za uzalishaji.
Kutumia mtaji wake katika kufanikisha program hii ya kukopesha wajasiriamali bila riba




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...