WATALAAM wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa  watafanya upimaji na matibabu ya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Iringa  na mikoa ya jirani.
Upimaji huo utafanyika kwa watoto na watu wazima tarehe 03/04/2023  hadi tarehe 07/04/2023  kuanzia saa mbili kamili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa.
Kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na  kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.
Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayebainika kuwa mgonjwa.
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa namba 0767054453 Dkt. Alfred Mwakalebela  Mkurugenzi wa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa  na 0657926892 Dkt. Faith Kundy .
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...