KAMPUNI ya Michezo ya kubashiri nchini Tanzania ya WinPrincess Bet imewapa ubalozi wasanii wawili wa ikiwemo wa vichekesho Lucas Mhuvile kwa jina maarufu ‘Joti’ na msanii wa Mziki wa Bongofleva Gift Stanford ‘Gigy Money’.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam wakati wakiwatangaza mabalozi hao, Meneja wa Mchezo wa Kubashiri wa WinPrincess nchini Hakan Aric, amesema kampuni imekuja kivingine kwa wateja wake kila atakayebeti kuanzia shilingi 1000 atajionea mwenyewe kwani ina zawadi nono hiyo ni kampeni mpya ya “Ushindi Papo Hapo” (“Immediate Pay-Out”) katika kuweka dau mtandaoni.
“WinPrincess Online Platform inakaribisha watu wote wazoefu na wapya kubashiri kwa njia ya mtandaoni kupitia kampuni hii yenye jumla ya uzoefu wa miaka saba katika kwa kuweka Dau kwenye simu popote mtu alipo mtandaoni,” amesema Aric na kuongeza,
“Kubashiri michezo ya mpira na kasino kupitia tovuti ya WinPrincess inakuja na faida nyingi ambazo huleta msisimko wa kweli ikiwemo kuanzia kubashiri kwa kima cha chini hadi shilingi moja ambayo ni nafuu kwa kila Mtanzania kuanzia miaka 18 na kuendelea, kampuni hii ina odds kubwa kuliko zile zilizopo hapa nchini,”.
Ameongeza “Ikiwa na lengo la kujali maslahi ya wateja, kuwapa ofa ya asilimia 100 kwa kila mchezaji mpya, uwezo wa kubet mchezo mmoja hadi arobaini, kutoa bonasi kupitia bahati nasibu zetu na bonasi za kurejesha pesa yote pamoja na mpango wa uaminifu unaoturuhusu kuwatuza wateja wetu wa kwa waaminifu bila longolongo
Aric amemshukuru James Mbalwe ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania kwa kutuma mwakilishi kuwa nao katika siku yao muhimu, ambapo pia ameishukuru Africa Princess Casino ambayo ni kampuni dada yao kwa kuwa mwekezaji wao..
Naye Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Regaliva Martini amewashairi Watu wote wanaoenda kubeti kuwa na kiasi na kuwa makini kwani Kuna muda wa kufanya kazi za kujiingizia kipato hivyo watumie muda wao vizuri
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Tele-Marketing kutoka WinPrincess Sports Betting, Winny Macha amesema amesema wanamatarajio makubwa sana jamii itawapokea kwani wamekuwa kila mwisho wa mwaka wanadisha shukrani Kwa Jamii Kwa kutembelea vituo mbalimbali vya watoto yatima Kwa kutoa misaada hivyo .
“Sisi kama WinPrincess tunaamini katika uaminifu na tuko hapa kutoa imani kwa wateja wetu kwa kutangaza kauli mbiu yetu “Ushindi ni Papo Hapo” ambayo ina maana mshindi ana uhakika wa Malipo Papo Hapo kutokana na ushindi wake,”.
Ameongeza “Tuanapoadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake, tunapenda kuwakaribisha wanachama wapya, hasa wanawake kuja kujaribu jukwaa letu na kujiburudisha kwa hali ya kawaida ya kushinda na kupata zaidi. Odds Bora na Malipo Papo Hapo,”.
Naye Msanii Gigy Money ameshukuru kwa kupewa ubalozi huo ambapo ameahidi kuitangaza na kuhakikisha wateja wapya wanapatikana hivyo wanawake vijana watoto na makundi yote waitumie kampuni hiyo kubashiri ina zawadi nono
Aidha Meneja wa Msaanii Joti ambaye ni Peter Mkoba ameshukuru kampuni hiyo kwa kumuamini Joti na kumfanya kuwa balozi ambapo ameeleza kuwa Joti ataitangaza kwa nguvu zake zote.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...