Mhandisi Lightness Salema ambaye ni Mkurugenzi wa Kipindi Thamani Madini Limited akimhudumia mteja aliyefika kununua bidhaa kwenye banda hilo katika maonesho yanayoendelea Mlimani City Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa TWCC Mwanaidi Hamza akizunguma na wajasiriamali hawapo pichani kwenye Ukumbi wa Mikutano Mlimani City Jijini Dares Es Salaam leo.
Makamu Mwenyekiti wa TWCC, Victoria Mwanukuzi akikata keki huku shuhudiwa Mlurugenzi wa TWCC Mwajuma Hamza na wageni wengine meza kuu.
Makamu Mwenyekiti wa TWCC Victoria Mwanukuzi (aliyevaa gauni ya bluu bahari) na Mkurugenzi wa TWCC Mwajuma Hamza wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya wazawa ya Azania ambao wanashiriki kwenye maonesho hayo ya wajasiriamali.

Na Khadija Kalili, Michuzi TV
MAKAMU MWENYEKITI wa Chama Cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Victoria Mwanukuzi ametoa wito kwa watanzania wote kuthamini na kununua bidhaa za ndani kwani ndiyo njia kubwa ya kuweza kuzipandisha thamani na kukuza uchumi wa wajasiriamali na wafanyabiashara kwa ujumla.
Makamu Mwenyekiti Mwanukuzi amesema hayo leo Machi 10,2023 alipokua akizungumza kwenye kongamano la wajasiriamali na wafanyabiashara wanawake katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
"Tumekutana leo ikiwa ni katika muendelezo wa kusherehekea siku ya Mwanamke Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka....,siku hii sisi tumeiita siku ya wajasiriamali wa Afrika na bado tunaendelea kusherehekea pamoja hivyo nawasisitiza tupende kununua bidhaa za nyumbani kwa sababu zina ubora madhubuti kushinda hata hizo bidhaa na ni za asili" amesema.
"Tuhamasishane kupenda vya nyumbani mimi binafsi nikiingia kufanya manunuzi kwenye maduka makubwa 'Super Market' huwa nanunua bidhaa zilizoandikwa Made in Tanzania yote hii ni kwa sababu ya kuwa na uzalendo" amesema Mwanukuzi.
Kwa upande wake, Mhandisi Lightness Salema ambaye pia ni miongoni mwa wajasiriamali amesema kuwa wakati umefika wa mjasiriamali ili anyanyuke lazima ajinyanyue mwenyewe ndipo atainuliwa na kusogezwa huku akisisitiza lazima mwanamke awe mwaminifu kwenye biashara kwa ujumla.
Naye, Mkurugenzi wa TWCC Mwajuma Hamza amesisitiza kuwa hivi sasa tunaelekea katika soko huru la Afrika hivyo wajasiriamali ni wajibu wao kujituma na kujikuza ili kuweza kukabiliana na ushindani wa biashara wakati utakapo fika licha ya kuwa wanakabiliana na changamoto mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...