
Atoa wito kwa wananchi kuitumia
Na John Mapepele
Serikali imewataka wananchi wote nchini kutumia boti ya kisasa ya Utalii iliyozinduliwa rasmi leo ili kukuza utalii wa ndani.
Kauli
hiyo ameitoa Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa
Kilwa Masoko kwenye hafla ya uzinduzi wa boti maalum ya Utalii
ijulikanayo kama TAWA SEA CRUISER inayomilikiwa na Mamlaka ya Usimamizi
wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Mhe.
Mchengerwa amefafanua kuwa boti hiyo itakuwa ikifanya safari katika
ukanda wote wa Pwani ili wajionee vivutio mbalimbali vya utalii.
Amevitaja
baadhi ya vivutio vya utalii vinavyopatikana katika eneo la Kilwa kuwa
ni pamoja na misitu ya matumbawe, kasa, mikoko, na samaki wa aina
mbalimbali.
Katika
hatua nyingine Mhe. Waziri ametembelea maeneo ya kitalii ya mji mkongwe
wa kihistoria wa Kilwa na kujionea vivutio vya utalii vya asili kama
msikiti wa Karne ya 12 magofu ya kale na jumba la mfalme.
Akiwa katika msikiti wa kale ameiagiza Bodi ya TAWA kuona namna ya kuboresha mji huo ili kuvuta watalii wengi.
Pia
Kisiwani hapo Mhe Mchengerwa ameshuhudia boti ya kisasa ya Le Jacques
Cartier Ponant kutoka nchini Ufaransa ikitia nanga katika fukwe ya Kilwa
Kisiwani na baada ya muda mfupi kuanza kuwashusha wageni.
Boti
hiyo ni ya tatu katika kipindi cha wiki moja tushusha wageni ambapo
boti ya kwanza ya Coral Geographer kutoka Australia ilishusha wageni 120
Machi 7 mwaka huu ikafuatiwa na Meli hii hii Machi 9 iliyoshusha pia
watu 110 na hii ya leo iliyoshusha wageni 93 kutoka nchini Ufaransa.









Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...