Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) ilikutana tarehe 14 Machi 2023, kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa sera ya fedha katika miezi Januari na Februari 2023,mwenendo wa uchumi, na kufanya maamuzi ya mwelekeo wa utekelezaji wa sera ya fedha kwa miezi miwili ijayo. Kamati iliridhishwa na utekelezaji wa sera ya fedha iliyolenga kupunguza ongezeko la ukwasi kwenye uchumi ili kukabiliana na kasi ya mfumuko wa bei nchini.
Kufuatia utekelezaji thabiti wa sera ya fedha, mfumuko wa bei
umeendelea kubakia ndani ya malengo, na kiwango cha ukwasi kikiendana na
mahitaji halisi ya shughuli mbalimbali za kiuchumi, hali iliyochochea ongezeko la
ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi, na kuweka mazingira ya kuendelea kuimarika
kwa shughuli za kiuchumi nchini.

Vilevile, utekelezaji huu wa sera ya fedha umesaidia kufikiwa kwa vigezo vilivyowekwa katika makubaliano ya programu na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) chini ya Mpango wa Extended Credit Facility (ECF) kwa mwezi Desemba 2022, na kuendelea kupunguza athari za kiuchumi zitokanazo na mitikisiko ya kiuchumi duniani, hususan athari za ongezeko la bei za bidhaa katika soko la dunia.
Kuhusu mwenendo wa uchumi, Kamati ilibaini kuwa mwaka 2022 uchumi wa dunia uliathiriwa na mitikisiko ya kiuchumi na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi. Kutokana na haya, kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia inatarajiwa kupungua mwaka 2023, kabla ya kuongezeka tena mwaka 2024. Bei za bidhaa katika soko la dunia ziliendelea kuwa juu katika mwaka 2022, japo zilianza kupungua katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka. Kutokana na hali hiyo, mfumuko wa bei umeendelea kupungua tangu robo ya mwisho ya mwaka 2022, japo umebaki juu ya malengo ya benki kuu za nchi nyingi, hususan mataifa yaliyoendelea. Aidha, Kamati ilibaini kuwa:
i. Mwenendo wa uchumi nchini umeendelea kuwa wa kuridhisha, huku viashiria
mbalimbali vya shughuli za kiuchumi vikionesha matarajio chanya kwa kipindi
kijacho. Kwa kuzingatia kasi ya wastani wa ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.2
katika robo tatu za kwanza za mwaka 2022 kwa Tanzania bara, kuna uwezekano mkubwa ukuaji wa uchumi ukafikia asilimia 5 kwa mwaka 2022,
kiwango ambacho ni juu ya makadirio ya awali ya ukuaji wa asilimia 4.7.
Kwa upande wa Zanzibar, uchumi unakadiriwa kukua kwa asilimia 5.4 mwaka 2022,kutokana na jitihada zinazoendelea katika kuimarisha uchumi wa buluu,
kuimarika kwa shughuli za utalii, pamoja na sera madhubuti za fedha na
kibajeti.
kibajeti.
Kamati inatarajia ukuaji wa uchumi kuendelea kuimarika zaidi ndani ya
mwaka 2023 kutokana na ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi, jitihada
mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kuboresha mazingira
ya biashara na uwekezaji nchini, kuimarika kwa shughuli za utalii, na utekelezaji
wa sera madhubuti za fedha na kibajeti. Hali hiyo itachagizwa pia na matarajio
ya kupungua kwa shinikizo la mfumuko wa bei na kuimarika kwa mnyororo ya
ugavi duniani;

ii. Mfumuko wa bei umeendelea kuongezeka katika miezi ya hivi karibuni,
kutokana na athari ya vita inayoendelea nchini Ukraine, ambayo imesababisha
ongezeko la bei za bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi. Mfumuko wa bei
kwa Tanzania bara uliongezeka na kufikia asilimia 4.9 mwezi Januari 2023,
kutoka asilimia 4.8 mwezi uliotangulia, kiwango ambacho kimeendelea kubakia
ndani ya lengo la nchi la asilimia 5.4 kwa mwaka 2022/23, na vigezo vya
mtangamano vya nchi wanachama wa EAC na SADC vya asilimia 8 na asilimia
3 hadi 7, mtawalia.
Kwa upande wa Zanzibar, mfumuko wa bei uliongezeka na
kufikia asilimia 8.4, kutokana na ongezeko la bei za chakula na bidhaa zisizo
za chakula. Aidha, Kamati inatarajia mfumuko wa bei nchini kubaki ndani ya
lengo katika nusu ya pili ya mwaka 2022/23 kutokana na matarajio ya
kuendelea kupungua kwa bei za bidhaa na mfumuko wa bei katika nchi
washirika wa biashara, pamoja na matarajio ya kuongezeka kwa uzalishaji wa
mazao ya chakula nchini.

Kupungua huku kutachagizwa pia na utekelezaji
thabiti wa sera ya fedha inayolenga kupunguza kiwango cha ongezeko la
ukwasi kwenye uchumi unaofanywa na Benki Kuu;
thabiti wa sera ya fedha inayolenga kupunguza kiwango cha ongezeko la
ukwasi kwenye uchumi unaofanywa na Benki Kuu;
iii. Ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) ulikua kwa asilimia 12.8 katika
mwaka ulioshia Januari 2023, sanjari na lengo la asilimia 10.3 kwa mwaka
2022/23. Hali hii ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na ukuaji mzuri wa mikopo kwa
sekta binafsi uliofikia takriban asilimia 23;
mwaka ulioshia Januari 2023, sanjari na lengo la asilimia 10.3 kwa mwaka
2022/23. Hali hii ilichangiwa kwa kiasi kikubwa na ukuaji mzuri wa mikopo kwa
sekta binafsi uliofikia takriban asilimia 23;
iv. Katika miezi saba ya kwanza ya mwaka 2022/23, utekelezaji wa bajeti za
Serikali umeendelea kufanyika kuendana na malengo. Mapato ya ndani
yalifikia asilimia 97.1 na asilimia 96.1 ya malengo kwa Tanzania Bara na
Zanzibar, mtawalia. Mwenendo huu umechangiwa na kuimarika kwa mifumo
ya usimamizi wa ukusanyaji mapato na utayari wa walipa kodi. Aidha, matumizi
ya Serikali yalifanyika kulingana na rasilimali zilizopo, sanjari na uhitaji wa
kuimarisha miundombinu nchini na jitihada za Serikali za kuunusuru uchumi
kutoka katika athari za misukosuko ya kiuchumi duniani kwa lengo la
kuhakikisha ukuaji wa uchumi unakuwa shirikishi na endelevu;

v. Sekta ya nje imeendelea kuathiriwa na misukosuko inayotokana na vita
inayoendelea nchini Ukraine na athari za janga la UVIKO-19. Changamoto hizi
zilipelekea kuongezeka kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na
uhamisho mali nchi za nje, kufikia dola za Marekani bilioni 5.2 mwaka ulioishia
mwezi Januari 2023, ikilinganishwa na nakisi ya dola za Marekani bilioni 2.6
mwezi Januari 2022, kutokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa katika soko
la dunia.

Akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani bilioni 4.8 mwishoni
mwa mwezi Januari 2023, kiwango kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na
huduma kutoka nje ya nchi kwa miezi 4.3, ikilinganishwa na lengo la nchi la
miezi isiyopungua minne. Katika vipindi vijavyo, urari wa biashara ya bidhaa,
huduma na uhamishaji mali nchi za nje, pamoja na idadi ya miezi ya uagizaji
wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi, vinatarajiwa kuimarika kutokana na
kuendelea kuimarika kwa mnyororo wa ugavi na matarajio ya kupungua kwa
bei za bidhaa katika soko la dunia;

vi. Sekta ya benki imeendelea kuwa thabiti, yenye kiwango cha kutosha cha mitaji,ukwasi, na yenye kutengeneza faida. Rasilimali za sekta ya benki na amana
ziliendelea kuongezeka kutokana na kuimarika kwa shughuli za kiuchumi,
pamoja na ongezeko la matumizi ya huduma za uwakala wa mabenki na
huduma za fedha kidijitali.
ziliendelea kuongezeka kutokana na kuimarika kwa shughuli za kiuchumi,
pamoja na ongezeko la matumizi ya huduma za uwakala wa mabenki na
huduma za fedha kidijitali.
Aidha, rasilimali za sekta ya benki zimeendelea kuboreshwa, zikiakisiwa na kupungua kwa kiwango cha mikopo chechefu hadi kufikia asilimia 5.85 mwezi Januari 2023, kutoka asilimia 8.42 mwezi Januari 2022;Kwa kuzingatia mwenendo na matarajio ya uchumi wa ndani na nje ya nchi, Kamati ya Sera ya Fedha imeridhia Benki Kuu ya Tanzania kuendelea na utekelezaji wa sera ya fedha inayolenga kupunguza kiwango cha ukwasi katika uchumi kwa mwezi Machi na April 2023.
Msimamo huu wa sera ya fedha unalenga kuhakiksha kuwa mfumuko
wa bei unabakia ndani ya lengo la asilimia 5.4, na kuendelea kuchochea kuimarika kwa shughuli za uchumi nchini. Vilevile, sera hii ya fedha itasaidia kufikiwa kwa malengo yaliyoainishwa kwenye programu ya IMF chini ya mpango wa ECF kwa mwezi Machi na Juni 2023.

Aidha, Benki Kuu itaendelea kuweka mazingira ya kisera yatakayowezesha kufikiwa kwa malengo mapana ya kiuchumi ya Serikali, na kufuatilia kwa karibu mwenendo mzima wa vihatarishi mbalimbali vinavyotokana na misukosuko ya kiuchumi duniani, na kuchukua hatua stahiki pale itakapohitajika.
GAVANA
BENKI KUU YA TANZANIA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...