Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (Mewata) kimefanya kongamano kubwa la kisayansi la kujadili changamano za masuala ya afya hususani saratani ya kizazi na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Kongamano hilo ambalo
limekutanisha madaktari, wanasayansi na wadau mbalimbali wa masuala ya
afya lilifanyika Dar es Salaam jana katika Ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere na kufunguliwa na Waziri wa Afya za
Zanzibar, Nassoro Ahmed Mazrui.
Kongamano hilo litafuatiwa na
Mkutano Mkuu wa 20 wa Mewata utakaofanyika kesho katika ukumbi huo ikiwa
ni maadhimisho ya miaka 35 tangu kuanzishwa kwa chama hicho kisicho cha
kiserikali, ambacho malengo yake makuu ni kusaidia, kuhamasisha na
kutoa elimu mbali mbali zinahusiana na magonjwa na afya ya mama na
mtoto.
Akizungumza
wakati wa kongamano hilo, Rais wa Mewata,Zaituni Bokhary alísema Mewata
imejikita katika kupambana na magonjwa ya saratani yanayoshambulia
wanawake kwa asilimia kubwa, hususan saratani ya mlango wa kizazi, na
saratani ya matiti.
Alisema pia kinahamasisha watoto wakike
kujiunga na fani za udaktari ili baadae wawe madaktari kwani huko nyuma,
fani ya udaktari ilikuwa ni kwa ajili ya wanaume tu, hatua ambayo
imeleta mafanikio makubwa kwani sasa kuna idadi ya kutosha ya madaktari
wanawake na inaendelea kukua.
Bokhary
alisema chama hicho kimefanya mazoezi ya kupima afya za kina mama
katika mikoa mbalimbali nchini ikiwamo, Dar es Salaam, Mbeya, Lindi,
Mtwara, Kilimanjaro, Njombe, Iringa, Tabora, Dodoma, Songea na Mwanza.
“Katika
mazoezi haya, tulifanikiwa kuwafanyia uchunguzi wa awali wa saratani ya
matiti wakina mama takriban 73,744, na uchunguzi wa saratani ya shingo
ya kizazi kina mama 9,307. Tuligundua kina mama wengi wana matatizo
mengi ya kiafya hususan magonjwa ya saratani na uelewa mdogo wa maradhi
haya.
Hii
ilipelekea wamama wengi kuripoti hospitali wakiwa wamechelewa au wako
katika hatua za mwisho za ugonjwa na kuchangia vifo vingi vitokanavyo na
saratani kwa kina mama’ alisema.
Aisha, alisema pamoja na hilo,
Mewata kwa kushirikiana na serikali imefanikiwa kuhamasisha wanafunzi wa
kike wa sekondari kuchukua masomo ya sayansi na kuongeza idadi ya
madaktari wanawake Tanzania na pia kimeweza kuwajengea uwezo madaktari
na kupelekea kuteuliwa kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali na
taasisi binafsi.
Katika hatua nyingine, profesa Mwaikambo
alisema Mewata ina mpango wa kujenga hospitali katika eneo la Mbweni,
Dar es Salaam kwa msaada wa serikali ya Japan kupitia mama mlezi wa
chama, mama Salma Kikwete.
“Kwa sasa tumehamasishana wanachama na
tumeweza kukusanya kiasi cha shilingi milioni 31,530,000 za kitanzania
fedha taslim na milioni 46,530,000 zikiwa ni ahadi” alisema.Rais huyo wa
mewata alisema chama hecho kinatambua mchango mkubwa unaofanywa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupambana na vifo
vinavyotokea vya mama na mtoto, hivyo madaktari wanawake wanaunga mkono
juhudi zinazofanywa na Raisi Dk Samia Suluhu
Hassan.
“Tunatambua
Mheshimiwa Rais anapambanakatika kuhakikisha hakuna mama anayekufa kwa
sababu ya uzazi, hivyo amepeleka huduma muhimu karibu kabisa na makazi
ya watu.Aidha, Mewata inatambua mchango mkubwa unaofanywa na Mh Rais Dkt
Hussein
Ali Mwinyi katika kuboresha huduma za afya Visiwani Zanzibar kama kujenga na kuongeza vituo vya afya na kuboresha maslahi ya
madaktari” alisema.
Waziri
WA AFYA Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui akizindua kitabu kuhusu wasifu wa
mwasisi WA Chama Cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA), Profesa
Esther Mwaikambo (kulia) kwenye kongamano la 20 la Kisayansi la chama
jicho jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...