Na Jane Edward, Arusha

Mgomo wa siku mbili uliofanywa na Wafanyakazi wa kampuni ya kufua Vyuma na kutengeneza vifaa vya plastic ikiwemo matank Lodhia Group ya Jijini Arusha wamalizika Salama.

Wafanyakazi hao waligoma kushinikiza kudai masilahi kilio chao kimesikilizwa na uongozi wa kampuni hiyo na kuongeza mshahara na nyongeza za malipo ya masaa ya ziada kwa wafanyakazi wake .

Awali wafanyakazi takribani 700 wa Kampuni hiyo waligoma kufanya kazi kwa siku mbili kwa madai ya mshahara kuwa mdogo sana wa kiasi cha shilingi shilingi 150,000 ,vitendea kazi pamoja na mambo mengine.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika nje ya kiwanda hicho kikiwa chini ya kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Arusha mjini.

Mwenyekiti wa kiwanda cha LODHIA Arun Lodhia aliwataka wafanyakazi kurudi kazini ili kuendelea na kazi na kuahidi kukutana mara mbili kwa mwaka kuzungumzia changamoto za kiwanda kati ya wafanyakazi na menejimenti lengo likiwa ni kutaka kufanya kazi kwa ushirikiano .

"Mimi najua nilipoanzia maisha nilikuwa sina hata suruali wala mahala pa uhakika pa kulala siwezi kuona watanzania wenzangu mkipata changamoto nikanyamaza naagiza kuwepo kwa vikao vya mara kwa mara ili kuondoa changamoto zenu"Alisema Arun

Arun amesema kampuni imeamua kuongeza mshahara wafanyakazi kutoka shilingi 150,000 hadi shilingi 180,000 na kuahidi kulipa masaa ya ziada ,ili kila mmoja atimize majukumu yake bila kumuonea mtu.

"Kwa Wale wote waliochukuliwa hatua kwa kukosa kwenda kazini na kukatwa mshahara kampuni itawalipa pesa zao na kila kitu kiende sawa kwa kushirikiana lengo kila mmoja apate ugali wa familia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa Wilaya ambaye pia ni Mkuu wa wilaya Arusha,Felician Rutahengerwa aliwataka wafanyakazi kuendelea na kazi pamoja na kuacha tabia ya wizi sanjari na kutofika kazini kwa zaidi ya siku tatu bila Taarifa.

"Haki inakuja na wajibu ukitaka mshahara upande basi na wewe mfanyakazi utimize wajibu ili mwisho wa siku kiwanda kinufaike na wewe unufaike"Alisema Mkuu wa wilaya

Mmoja wafanyakazi wa Lodhia Group aliyejitambulisha kwa jina la Martin Antony alisema wanashukuru kwa busara iliyotumika ya kuweka sawa maslahi yao pamoja na kuondoa migogoro na kwamba wako tayari kuendelea na kazi.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Rutahengerwa akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha LODHIA cha jijini Arusha.
Kiwanda cha LODHIA jijini Arusha.
Viongozi wakisikiliza malalamiko ya wafanyakazi kiwanda cha LODHIA.

Mwenyekiti wa kiwanda cha LODHIA Arun Lodhia akizungumza na wafanyakazi wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...