MFANYABIASHARA Khamis Luwonga (38) anayetuhumiwa kumuua mke wake na kisha kuchoma mwili wake kwa magunia ya Mkaa, aneiomba mahakama imuachie huru kwa sababu mpaka sasa hakuna ushahidi wa kutosha kumshtaki.

Luoga anayekabiliwa na kesi ya mauaji namba 5, 2022 iliyoko katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amewasilisha ombi lake hilo mbele ya Jaji Bwagoge wa

Mahakama Kuu Masijala Kuu kupitia wakili wake, Mohamed Majaliwa akidai kuwa kesi iliyopo Kisutu inamapungufu kisheria.

Akiwasilisha hoja zake mbele ya Jaji Bwagonge, Majaliwa amedai kuwa, mteja wake (Luoga) anashtakiwa kwa kosa la mauji mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Rhoda Ngimilanga wa Mahakama ya Kisutu na kwamba kesi hiyo inaonekana mpya lakini kiuhalisia sio mpya kwa sababu kesi ya mauji namba 4,2019 dhidi ya mteja wake ilikwisha kumalizika.

Amedai mashtaka yaliyokuwepo kwenye hati hiyo yalipitia hatua zote za kisheria na Oktoba 24,2022 kesi iliitwa mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa ambapo upande wa mashtaka ulidai kuwa na mashahidi wanne.

Amedai kuwa, wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwasiti Ally alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga wa Mahakama ya Kisutu kuwa kesi iliitwa kwa ajili kusikilizwa, lakini Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya mshtakiwa.

Majaliwa akadai kutokana na kuomba kuondolewa kwa kesi hiyo, Hakimu Ruboroga alimuachia Luwonga, lakini cha kushangaza mshtakiwa alikamatwa tena na askari na baada ya saa chache baadae alipandishwa tena kizimbani na kusomewa mashitaka yale yale mbele ya Hakimu Ngimilanga

"Chakushangaza Mwasiti huyo huyo aliyeomba kesi namba 4,2019 kuondolewa ndiyo aliyemsomea mshitaka mapya mshtakiwa na kudai upelelezi bado haujakamilika, kwa hiyo mahakama ikatoa amri ya Luwonga kurudishwa rumande

Majaliwa ameendelea kudai kuwa, hadi leo jalada lililoko mbele ya mahakama hii linaonesha upelelezi bado haujakamilika, hivyo ni rai yao kwamba mashtaka mapya ni batili mbele yako kwa sababu yanakiuka sheria.

"Sheria imetoa utaratibu kama mtu akiachiwa na serikali ikataka kumshtaki tena basi ni lazima kuwepo na ushahidi wa kutosha na usikilizwaji wake uanze mara moja, lakini katika kesi hii hilo halijazingatiwa.

Wakijibu hoja hizo, upande wa mashtaka umedai kuwa mahakama hiyo imefungwa mikono kutoa amri kwenye amri ambazo hazijafika mwisho na pia uhalisia wa mashtaka ya mauaji ni lazima mshtakiwa awe komitedi

Katika hoja ya kuachiwa kwa mshtakiwa, upande wa mashtaka amedai hoja hiyo inakinzana na matakwa ya kisheria na pia taratibu za kisheria bado hazijakamilika kwa sababu kesi bado haijafika Mahakama Kuu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Baada ya Jaji kusikiliza hoja za pande zote mbili ameahirisha maombi hayo hadi Aprili 18, 2023 kwa ajili ya uamuzi. Mshtakiwa Luwoga anatetewa na wakili, Majaliwa Zidadi Mikidadi na Fatuma Abdul

Luwonga amefungua maombi Mahakama Kuu ili wapate maelezo ya uhalali wa kesi namba 5,2022 ya mauji baada ya kesi ya halali dhidi yake kufutwa na kufunguliwa upya.

Katika kesi hiyo ya muaji namba nne ya mwaka 2019, mshitakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam

Katika kesi hiyo inadaiwa, Mei 15, 2019 huko Gezaulole eneo la Kigamboni mshtakiwa Luwoga anayeishi Kigamboni jijini Dar es Salaam, alimuua Naomi Marijani na kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya Mkaa ambapo alichukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...